SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi na wadau mbalimbali wametembelea banda lao kujifunza shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 7,2023 Jijjni Dar es Salaam, Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi TBS, Bw. Gerald Magola amesema kongamano hilo lina ajenda mbalimbali na mojawapo ni kujadili masuala ya tabianchi ambayo yanahusiana na mambo ya chakula kwenye kilimo na uzalishaji.
Amesema wamehudhuria kongamano hilo kwaajili ya kuwezesha na kuwakaribisha wadau ili waweze kupata elimu mbalimbali kwaajili ya kupata huduma za Shirika la Viwango Tanzania ambazo zinahusiana na viwango.
Aidha amesema kuwa kila mwaka Serikali imekuwa ikitenga fedha kwaajili ya wajasiriamali wadogo waweze kupata huduma ya kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.
Pamoja na hayo amewakaribisha wazalishaji wa bidhaa na watanzania kwa ujumla kujifunza shughuli za TBS kwenye kongamano hilo ambalo linafikia tamati Seotemba 8,2023.
0 Comments