Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuiunga mkono Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara mwaka 2030 (EXPO 2030).
Ahadi hiyo imeelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo alipoelezea yaliyojiri katika mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mhe. Ahmed Abdulaziz Qattan uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Shelukindo amesema katika kikao hicho Mhe. Rais amemhakikishia mjumbe huyo maalum kuwa Tanzania itashiriki mkutano ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika Jijini Riyadh mwezi Novemba 2023.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia mjumbe huyo Maalum kuwa Tanzania itaiunga mkono Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 alisema Dkt. Shelukindo.
Balozi Shelukindo pia aliongeza kuwa Mhe. Rais amemhakikishia mjumbe huyo kuwa Tanzania itashiriki Mkutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika inayotarajiwa kufanyika Jijini Riyadh, Saudi Arabia mwezi Novemba 2023.
Naye Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mhe. Ahmed Abdulaziz Qattan amesema Saudi Arabia inaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali kuiunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 (EXPO 2030)
“Kwa niaba ya Serikali ya Saudi Arabia tunaishukuru sana Serikali ya Tanzania kwa kuahidi kutuunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka 2030 (EXPO 2030),” alisema Mhe. Qattan.
Aliongeza kuwa Saudi Arabia inamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kitendo cha kukubali Tanzania ishiriki katika Mikutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika Jijini Riyadh mwezi Novemba 2023
“Kwa niaba ya Serikali ya Saudi Arabia namshukuru Mheshimwa Rais kwa kukubali kutuunga mkono kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya EXPO 2030 na kukubali kushiriki mikutano kati ya Nchi za Kiarabu na Afrika (Afro Arab Summit) na Mkutano kati ya Saudi Arabia na Nchi za Afrika itakayofanyika Jijini Riyadh mwezi Novemba 2023,” aliongeza Mhe. Qattan.
Amesema katika kikao hicho wamejadili pia masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Saudi Arabia na Tanzania katika nyanja mbalimbali.
Tanzania na Saudi Arabi zimekuwa na uhusiano mzuri na zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali hususan utalii, biashara za bidhaa za nyama, matunda na mazao mengine ya chakula.
Mazungumzo baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mhe. Ahmed Abdulaziz Qattan yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akizungumza na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mhe. Ahmed Abdulaziz Qattan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mhe. Ahmed Abdulaziz Qattan wakieleza yaliyojiri katika mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe Maalum wa Mfalme wa Saudi Arabia Ikulu Jijini Dar es Salaam
0 Comments