Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 4 Septemba, 2023.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amemhakikishia Mhe.Biteko kuwa Bunge litampa ushirikiano wa kutosha ili kutimiza na kufanikisha shughuli za Serikali.
0 Comments