Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT.MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA KIISLAMU KATIKA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD VIWANJA VYA MAISARA SULEIMAN ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh,Saleh Omar Kabi (kushoto kwa Rais) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, baada ya kumalizika kwa Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023.(Picha na Ikulu)
SHEIKH.Said Nassor Said kutoka Magogoni Unguja akisoma Dua ya Barzanji wakati wa Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana usiku 27-9-2023 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Madrassatul Sufaiya kutoka Mwanakwerekwe Wilaya ya Mjini Unguja wakijumuika katika Maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Jumuiya ya Maulidi ya Homu kutoka Mtaa wa Mtendeni Wilaya ya Mjini Unguja, wakisoma Maulidi ya Homu katika Maadhimisho ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman jana usiku 27-9-2023.(Picha na Ikulu)
USTADH Omar Abdi Abdulla kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu akisoma Khutba ya Maadhimisho ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar jana usiku 27-9-2023.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Madrassatul Sanaa Muntakaa Kalam kutoka Ukongoroni Wilaya ya Kati Unguja wakisoma Qaswida, katika Maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 27-9-2023.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments