Ferdinand Shayo ,Manyara .
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amepongeza uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha vinywaji vikali cha Mati Super Brands Limited kilichopo Wilayani Babati Mkoani Manyara ambacho kimekua mstari wa mbele katika ulipaji kodi kwa serikali pamoja na kujitoa kusaidia jamii inayowazunguka kwa kutoa misaada mbali mbali.
Akizungumza mara baada ya kutembea kiwanda cha Mati Super Brands Limited,Mkuu wa Mkoa wa Manyara amepongeza kiwanda hicho kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana wa Mkoa wa Manyara .
"Sisi kama serikali tunawapongeza kwa ulipaji mzuri wa kodi za serikali ambao unachangia Maendeleo kwa taifa kwa ujumla kalini pia mmekua mstari wa mbele kujitolea katika masuala ya kijamii" Anaeleza Queen Sendiga.
Sendiga amesema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili waweze kufanya kazi zao bila usumbufu wowote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited David Mulokozi amepongeza serikali ya Awamu ya Sita ya Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora kwa wawekezaji na wafanyabiashara.
"Kwa sasa tuna serikali imeweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi ambayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya kazi na kulipa kodi kwa hiyari" Anaeleza Mulokozi
0 Comments