MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia Mkutano wa Kimataifa Unaojadili Mfumo wa Chakula,unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023, na (kulia kwake) Waziri wa Maendeleo anayeshuhulikia Masuala ya Kimataifa wa Norway Mhe.Anne Beathe Tvinnereim na (kushoto kwake) Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika ( AGRA) Dkt.Agnes Kalibata.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar.Mama Mariam Mwinyi akizungumza na kutoa Mada juu ya nafasi ya Mwanamke katika Kilimo, wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Mfumo wa Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023(AGRF) linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Mkutano wa Kimataifa Unaojadili Mfumo wa Chakula, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo 6-9-2023.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika ( AGRA) Dkt. Agnes Kalibata, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi mdogo wa jengo la Mikutano la Kimataifa la Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu, kabla ya kuaza kwa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF) uliyofanyika leo 6-9-2023 katika ukumbi huo.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe. Ummy Nderiananga na Rais wa Jumuiya ya Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA) Dkt. Agnes Kalibata, alipowasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaamu kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF) lililofanyika leo 6-9-2023, katika ukumbi huo.(Picha na Ikulu)
0 Comments