Ticker

6/recent/ticker-posts

KONGAMANO LA KWANZA LA KIMATAIFA LA INSIA LA AFRIKA 2023 KUFANYIKA SEPTEMBA 13-15,2023 UDSM

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, kupitia Ndaki yake ya Insia wameandaa Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Insia la Afrika 2023 ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 13 hadi 15,2023 katika Kampasi yake ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mlimani Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Kongamano hilo, Prof.Gastor Mapunda amesema kongamano hilo ni tukio la kitaaluma ambalo litawakutanisha wasomi, watafiti na watendaji kutoka taasisi mbalimbali, vyuo vikuu, mabaraza ya Insia, Viwanda, na Umma kutoka ndani na nje ya ukanda wa Afrika.

Amesema kuwa Mada Kuu ya Kongamano hilo ni "Kuadhimisha Insia Afrika kwa Ukuaji Jumuishi" na itagawanyika katika mada ndogondogo kwa minajili ya kutuhusu utangamano wakitaaluma na ubadilishanaji maarifa. Mada zitakazowasilishwa ni 135 na washiriki wanatoka katika mataifa 17.

"Mada kuu zitatolewa na wasomi mashuhuri ambao uwasilishaji wao utakuwa na mwelekeo wa insia ulimwenguni na uhuishaji wake katika bara la Afrika". Amesema Bw. Mapunda

Aidha Bw. Mapunda amesema Kongamano hilo limefanikishwa kwa hisani ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na wadau kama Benki ya CRDB, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Mwenyekiti wa Kamati ya Kongamano Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Insia la Afrika 2023, Prof.Gastor Mapunda akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10,2023 Jijini Dar es Salaam.
Rasi, Ndaki ya Insia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Rose Upor akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10,2023 Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments