Ticker

6/recent/ticker-posts

DC MAGEMBE AFUNGUA MAFUNZO YA KUONGEZA UELEWA WA MADHARA YA MATUMIZI YA ZEBAKI KWA WACHIMBAJI WADOGO

ONGEZEKO la wachimbaji wadogo nchini litakwenda sambamba na ongezeko la uharibifu wa mzingira na matumizi ya kemikali za zebaki hali ambayo inaweza kupelekea kuwepo kwa athari katika afya ya jamii na uharibifu wa mifumo ya ikolojia.
Ameyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Cornel Magembe wakati akifungua Semina ya Matumizi Sahihi Ya Teknolojia katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira yaliyofanyika mkoani Geita.

Mhe.Magembe amesema kuwa tunapaswa kuchukua tahadhari kabla ya athari kutokea ili kukidhi matakwa ya Serikali katika kufanikisha azma ya kupunguza uchafuzi utakanao na matumizi endelevu ya rasilimali.

Aidha amewapongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kuwaleta wadau wengine kama Mkemia Mkuu wa Serikali, STAMICO na Wizara ya Afya katika kutoa elimu juu ya afya ya Jamii na utunzaji wa Mazingira katika Mkoa wa Geita na wachimbaji kwa ujumla.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki Tanzania Befrina Igulu amesema mradi huo wenye lengo la kutafiti juu ya teknolojia mbadala zilizoko nchini na zile ambazo zinafanyiwa tafiti mbalimbali na kuzifanyia majaribio na hatimaye zitasambazwa kwa wachimbaji wadogo hapa nchini na kuwapa elimu juu ya matumizi yake kwa lengo la kuwafanya waondokane na matumizi ya zebaki.

"Kupitia Mradi huu tutaweza Kupitia Sheria na Kanuni zilizopo na kuziboresha kwa kuingiza vipengele vitakavyowezesha usimamizi thabiti wa uingizaji, utunzaji utumiaji na zebaki nchini pamoja na masuala ya uteketezaji". Amesema

Amesema kupitia mradi huo, elimu itatolewa kwa wananchi hususan wachimbaji wadogo kuhusu madhara ya zebaki na namna bora ya kuitumia bila kuathiri afya na mazingira.

"Sambamba na elimu itakayotolewa kwa wananchi, na sie wenyewe pia tunapaswa kuhakikisha tumekuwa na uelewa sawa wa matakwa ya mikataba ya Minemata na Basel yenye lengo kuu la kupunguza matumizi ya zebaki Nchini". Ameeleza




Post a Comment

0 Comments