Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda amewaomba wananchi wa Mbarali kumpa kura za ndio, Bahati Ndingo ambaye ni mwanamke msikivu ,mpenda maendeleo makubwa katika kukuza uchumi wa Mbarali mkoani Mbeya.
Mwenyekiti Chatanda amesema, 'Sisi kama wanawake Wilaya ya Mbarali tuwaombe wanaume zetu usiku na mchana katika kuunga juhudi za mwanamke kwa kumpa kura za ndio Mgombea wetu wa Ubunge Jimbo la Mbarali.
"Mwanamke ndio Jeshi la familia na niwahakikishie mmepata mwanamke shupavu na atawaongoza kikamilifu ndani ya Wilaya yetu msifanye makosa chagua Bahati Ndingo kwa Maendeleo ya Mbarali.
"Mimi kama Mwenyekiti wetu wa Wanawake Tanzania niwaombe wananchi wa Mbarali ifikapo tarehe 19/9/2023 msifanye makosa mchague Chama Cha Mapinduzi ,mchague mgombea Bahati Ndingo awe Mbunge wa Mbarali".
0 Comments