Ticker

6/recent/ticker-posts

BARAZA LA 12 LA UONGOZI NIT LA AHIDI KUTOA USHIRIKIANO KWA MENEJIMENTI YA CHUO

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Uongozi jipya la 12 la Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) limeipongeza Baraza la 11 lililomaliza muda wake kwa kufanya kazi kubwa na Maendeleo kuzidi kuonekana.

Pongezi hizo zimetolewa leo Septemba 30, 2023 Jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi Jipya la 12 Mwenyekiti wa Baraza la 12 la Uongozi wa Chuo, Prof. Ulingeta Obadiah Mbamba amesema kuwa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye miundombinu ya usafirishaji, hivyo hawana budi kufanya kazi ya ziada katika kuhakikisha wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kwenye sekta ya usafirishaji.

Aidha ameishukuru menejimenti ya Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) kwa kuendelea kufanya vizuri, hivyo baraza lipo kwaajili ya kusaidia na maendeleo yaweze kuonekana.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la 11 la Uongozi wa Chuo, Mhandisi Eliona Simbo, akiongea kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza , amesema kwa kipindi walichokuwepo walipata ushirikiano mkubwa na menejimenti ya Chuo hivyo kufanya kuonekana kwa maendeleo chuoni hapo

"Haya maendeleo yanayoonekana, hatuna budi kuishukuru menejimenti ya Chuo kwa ushirikiano mkubwa walioutoa pindi tunapoingia kazini kwa mara ya kwanza hadi kufikia mwisho na kuchaguliwa kwa Baraza lingine". Amesema

Nae Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa amesema uanzishwaji wa Kituo cha Mafunzo ya Usalama Barabarani ambacho kinafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika ni moja ya mafanikio yaliyopatikana katika Uongozi wa Baraza la 12.

" Kutokana na wingi wa matukio ya ajali barabarani, kituo hiki kimedhamiria kupunguza ajali za barabarani". Amesema Prof.Mganilwa.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi Jipya la 12 Dkt.Dina Zawadi Machuve (kulia) akipokea vitendea kazi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la 11 lililopita Mhandisi Dkt. Gemma Modu katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Baraza la 12 la Uongozi wa Chuo, Prof. Ulingeta Obadiah Mbamba akizungumza katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la 11 lililopita Mhandisi Dkt. Gemma Modu akizungumza katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es SalaamMjumbe wa Baraza la 11 la Uongozi wa Chuo, Mhandisi Eliona Simbo akizungumza katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa akizungumza katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi Jipya la 12 Dkt.Dina Zawadi Machuve (kulia) akikabidhi zawadi kwa Wajumbe wa Baraza la 11 la Uongozi wa Chuo katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam
la Uongozi jipya la 12 la Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Baraza la 12 la Uongozi wa Chuo, Prof. Ulingeta Obadiah Mbamba akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la 12 la Uongozi wa Chuo na Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake wakati wa hafla ya kuliaga Baraza hilo leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO))

Post a Comment

0 Comments