Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI KIJAJI AIAGIZA BRELA KUWEKA KAMBI MKOANI ARUSHA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ,akizungumza na wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kusikiliza changamoto walizonazo na kuzitatua

Na.Mwandishi Wetu-ARUSHA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ameiagiza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuweka kambi Mkoani Arusha kwa lengo la kurasimisha wafanyabiashara wa kilimo ili wapate leseni, tini na vibali vya kusafirisha mazao nje ya nchi.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Agosti 1, 2023 alipokutana na wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kusikiliza changamoto walizonazo na kuzitatua

Aidha, Dkt Kijaji amewaonya wafanyabiashara wazawa kuacha mara moja tabia ya kukata leseni na kuwauzia wageni wanaokuja nchini kununua mazao hadi mashambani badala ya kuyafuata kwenye masoko husika

Amesema endapo wafanyabiashara wa mazao wakirasimishwa na kupata leseni zao wataweza kutambulika, idadi yao itajulikana ili kurahisisha jitihada za kuwakwamua kiuchumi wafanyabiashara na wakulima wanauza mazao ya nafaka mbalimbali nchini.

Waziri Kijaji pia amebainisha kuwa Serikali iko mbioni kufuta vibali vya usafirishaji wa mazao vinavyokatwa kila mkoa badala yake kibali kiwe kimoja tu kilicholipiwa kila kitu ili kuwezesha wafanyabiashara wa mazao kubeba mizigo yao na kupelekea mahali husika bila kukata vibali kila Mkoa wanapopita.

Aidha amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita haiko tayari kuwakwamisha wafanyabiashara na wawekezaji kushindwa kufikia malengo yao bali itawasaidia kukua na kuendelea kibiashara, kukaa kwa pamoja na kutatua changamoto zao ili kuhakikisha ufanyaji biashara wao unakuwa na tija na manufaa kwa Taifa .

Dkt. Kijaji amesema ameridhishwa na uwekezaji huo ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya matumizi ya Vishkwambi katika shule za awali na zile za sekondari ambapo vitasaidia kufundisha wanafunzi namna bora ya kutumia TEHAMA katika mitaala ya elimu

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda hicho cha Tanztech Bw. Gurveer Hans amesema Kiwanda hicho kipo tayari kushirikiana na Serikali katika kutoa bidhaa hiyo mashuleni na kwa watu binafsi kwa bei nafuu.

Awali Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wadogo(Machinga) Bi. Amina Samson Njoka akiongea mbele ya Waziri Kijaji amesema wafanyabiashara wadogo katika jiji hilo wamekuwa wakilalamika kuhusu tozo nyingi kutoka OSHA, Jeshi la Zimamoto, Idara ya Uhamiaji pamoja na Halimashauri ambazo zimekuwa kero na kuomba kiwa tozo hizo zitizwe zote mara moja.


Post a Comment

0 Comments