Ticker

6/recent/ticker-posts

USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI KWENYE UANDAAJI WA BAJETI KUPUNGUZA CHANGAMOTO KWENYE JAMII

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI yashauriwa uwepo ushirikishwaji wa wananchi katika mchakato wa uandaaji wa Bajeti ili kuondokana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza kutokana na ufinyu wa utekelezaji.

Ushauri huo umetolewa leo Agosti 23,2023 wakati wa Semina za Jinsia na Maendeleo zinazoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

Mwezeshaji Bw.Hansy Obote amesema wananchi kupitia viongozi ngazi ya kata wanatakiwa kushirikisha wananchi katika uandaaji wa bajeti ili wanachi waweze kueleza mahitaji yao na kuweza kutekelezwa.

Amesema katika mchakato huo basi wameshauri waanze kutoa muongozo ili wananchi wapate fursa kuibua mahitaji ambayo wananchi yanawagusa moja kwa moja.

Post a Comment

0 Comments