Tanzania ikiwa imeshafikia asilimia 37 kwenye uwiano wa viongozi wanawake ikiwa ni zaidi ya asilimia 1 ya malengo yakiowekwa, bado ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi ikowemo uongozi wa vyama pamoja na serikali umekuwa mdogo hususani katika ngazi za chini kwenye mitaa ambapo ushiriki wake ni asilimia 1.2.
Hayo yameelezwa jijibi Dar es salaam wakati wa semina ya siku tatu iliyoanza jana Augosti 4,2023 kwa viongozi wa dini na vyama vya vya siasa chini ya mtandao wa jinsia nchini TGNP.
Akizungunza katika ufunguzi wa Semina hiyo, Mkurugenzi wa TGNP Bi. Lilian Liundi amesema kwa sasa uwiano wa wabunge wanawake kwenye majimbo ni asilimia 9 huku madiwani wakiwa ni asilimia 6.58 ikiwa ni chini ya wanaume, hali inayoonekana kuchangiwa na kutotekelezwa kwa sera za vyama katika vyama vya siasa ambavyo ndivyo ngazi ya kushika uongozi.
Kwa upande wao viongozi wa dini Bw.Noah Lyanga kutoka Kanisa la EAGT Arusha pamoja na Rose Mwasubira wamesema sababu kubwa ya wanawake kutoshika nafasi za uongozi ni kutokana na mila potofu pamoja na kukosa uelewa juu ya elimu ya uongozi .
Nao baadhi ya wawakilishi wa vyama vya siasa akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA Bi.Sharifa Sulemani pamoja na Bw.John Mohamed kutoka CCM Tanga wamewataka wanawake kujiamini ili kuwania nafasi za uongozi katika ngazi za vyama na hivyo kupelekea uwepo wa wanawake wengi viongozi.
0 Comments