Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI KHAMIS ASHIRIKI MAZISHI YA BI. KHADIJA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameshiriki katika mazishi ya Marehemu Bi. Khadija Abbas Rashid aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1965, ambaye amefariki tarehe 22 Agosti, 2023 Zanzibar.

Mwili wa Marehemu Bi. Khadija umezikwa Bumbwini Makoba Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi ameshiriki pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Hanifa Selengu katika shughuli hiyo.

Marehemu Bi. Khadija aliyefariki nyumbani kwake Raha Leo Mkoa wa Mjini Magharibi atakumbukwa kwa kushiriki tukio hilo la kihstoria ambalo ni matunda ya Muungano huu imara.

Alishiriki tukio hilo la kuchanganya udongo akiwa umri wa miaka 16 pamoja na wenzake akiwemo Bw. Hassan Omar Mzee anayeishi Zanzibar, Bi. Sifael Mushi na Elisael Mrema kutoka mkoani Kilimanjaro.

Alitunukiwa Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano na Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia tarehe 26 Aprili, 2014.

Marehemu Bi. Khadija alizaliwa tarehe 23 Oktoba, 1949 na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Wasichana ya Forodhani - Unguja, ameacha watoto tisa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (katikati mwenye kanzu nyeusi) akishiriki ibada ya mazishi ya Marehemu Bi.Khadija Abbas Rashid mmoja wa walioshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1965, ambaye amefariki dunia tarehe 22 Agosti, 2023 Raha Leo Mkoa wa Mjini Magharibi na mazishi yake kufanyika Bumbwini Makoba, Mkoa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (wa nne kushoto mbele) akishiriki ibada ya mazishi ya Marehemu Bi.Khadija Abbas Rashid mmoja wa walioshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1965, ambaye amefariki dunia tarehe 22 Agosti, 2023 Raha Leo Mkoa wa Mjini Magharibi na mazishi yake kufanyika Bumbwini Makoba, Mkoa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments