Ticker

6/recent/ticker-posts

MAENDELEO BANK MARATHON KUKUSANYA MIL. 200

MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, William Kallaghe ameipongeza Benki ya Maendeleo plc kwa kuandaa mbio za hisani zenye lengo la kukusanya kiasi cha Tsh Mil. 200 kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa KCMC na Kituo cha watoto waliozaliwa na tatizo la afya ya akili yaani Usonji cha Mtoni Diakonia Dar es salaam.

Akizungumza leo Agosti 14, 2023 wakati wa uzinduzi wa ‘Kits’ za Maendeleo Bank Marathon 2023 jijini Dar es salaam MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, William Kallaghe amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuchangia kwenye Maendeleo Benki Marathon yenye nia ya kurudisha kwa jamii.

Aidha, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassimu Majaliwa anatarajiwa Kuwa mgeni Rasmi wa mbio za Maendeleo Benki Marathon zinazotarajiwa kufanyika Sept 2 Mwaka huu jijini Dar es Salaam zikiwa na lengo ya kuchangia matibabu ya matatizo usonji .

Hivyo, Dkt Mwangalaba amesema kuwa mbio hizo zitaenda sambamba na zoezi la uchangiaji wa Damu katika miaka kumi ya benki hiyo imeweza kupiga hatua na kufanikiwa kuwainua Watanzania.

"Katika miaka kumi yetu Benki imekuwa na wateja zaidi ya elfu 65000 ina Amana pia umeongezeka toka bilion 7 hadi bilioni 104" Amesema.

Pia unaweza kushiriki mbio za Maendeleo Benki Marathon zitakazofanyika tarehe 2, Septemba 2023 viwanja Farasi, OysterBay, unaweza kujisajili sasa kupitia tovuti ya events.maendeleobank.co.tz kwa ada ya Tsh 35,000 tu.

Post a Comment

0 Comments