Ticker

6/recent/ticker-posts

MAANDALIZI YA MAPOKEO YA MWENGE WA UHURU YAKAMILIKA KWA ASILIMIA ZOTE ,HAJJAT FATMA AZUNGUMZA NA WANA KAGERA .



**************

Na Shemsa Mussa , Kagera 

Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Hajjat Fatma Mwassa amekutana na waandishi wa habari leo kwa lengo la kuzungumza na wananchi kuhusu ujio wa Mwenge wa Uhuru mnamo tarehe 8/8/2023.

Hajjat Fatma amesema mandalizi yote yamekamilika kwa asilimia zote ikiwemo miradi mbalimbali itakayozinduliwa na kukaguliwa katika Mbio za Mwenge wa Uhuru.

"Yaani mambo yote yapo vizuri niwaakikishie wana kagera yamekamilika kwa asilimia 99.99 na asilimia iliyobaki ni ya kuchinja ng'ombe tu na msipange kukosa njoo kwa wingi,amesema Hajjat Fatma"

Aidha ameongeza kuwa miradi 57 itakaguliwa, kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika halmashauli zote 8 za mkoa wa kagera ikiwemo miradi ya barabara, Maji,Afya,na kilimo zilizoghalimu kiasi cha shiling Bilion 26.3




"Jumla ya miradi yote ni 57 na Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika wilaya zote zilizopo hapa kagera na utakimbizwa kilometa 1200.4 ameongeza Hajjat Fatma"




Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa katika wilaya ya Muleba mnamo tarehe 8 Agust 2023 na kukimbizwa wilaya za Mkoa kagera na Utakabidhiwa katika Mkoa wa kigoma mnamo tarehe 16 Agust 2023.

Post a Comment

0 Comments