Ticker

6/recent/ticker-posts

ATE, ILO WAKUTANA NA WADAU SEKTA BINAFSI KUJADILI MASUALA YA UKIMWI MAHALA PA KAZI

Mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba akizungumza katika mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini ( TUCTA), Bw. Herry Mkunda akizungumza katika mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam
Afisa Program Mwandamizi kutoka Shirika la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki (ILO), Bw. Edmond Moshi akizungumza katika mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam

Wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi wakiwa kwenye mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameandaa mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi.

Akizungumza katika Mkutano huo leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba amesema uwepo wa mkutano huo ni katika kutekeleza mpango mkakati wa Dunia wa kumaliza janga la UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

Amesema mchango mkubwa unaotolewa na ATE katika kuzikutanisha Sekta Binafsi na Wadau kupitia Programu mbalimbali za afya na masuala ya UKIMWI katika maeneo ya Kazi kwa kuzingatia Dunia iko katika mpango mkakati wa kumaliza janga la UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

"Pamoja na hatua kubwa ambazo Tanzania imepiga katika kutokomeza UKIMWI, bado kuna kazi kubwa ya kufanya na wadau wote ili kupata Tanzania isiyo na VVU/UKIMWI na kuwa ATE kwa kushirikiana na Serikali na Wadau wengine wataendelea kuunga mkono juhudi zote za kufikia lengo ifikapo mwaka 2030". Amesema Bi.Suzanne

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini ( TUCTA), Bw. Herry Mkunda ambaye pamoja na mambo mengine amewaomba wadau wote kuendeleza ushirikiano katika kuhamasisha masuala ya UKIMWI na Afya na Usalama mahala pa Kazi ili kufikia malengo ya mkakati wa 95% hadi kufikia mwaka 2030.

"Katika sehemu ya kazi tunatakiwa tulinde wafanyakazi kwasababu muajiri hawezi kupata faida kama wafanyakazi hawana afya nzuri kwahiyo pamoja na mambo mengine isiwe UKIMWI pekee bali hata magonjwa mengine yasiyoambukiza, hii itaweza kuondoa changamoto ya Afya sehemu ya kazi" Amesema

Pamoja na hayo amewaomba waajiri kuhakikisha wanaweka mipango ya kupambana na UKIMWI sehemu za kazi kama sehemu za bajeti zao lakini pia kuwe na utaratibu maalumu wa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza"

Kwa upande wake Afisa Program Mwandamizi kutoka Shirika la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki (ILO),Edmund Moshi alisema katika utekelezaji wa afya mbalimbali za eneo la afya bado kuna mambo mengi ya kufanya ikiwemo kuendeleza juhudi za kuhakikisha kwamba UKIMWI unaisha lakini pia pale ambapo upo watu wanaendelea kupewa msaada wanaohitaji ili kuendelea kuwa na Tija mahali pa kazi.

Mkutano huo umebeba kauli mbiu inayosema *“UKIMWI bado ni Ajenda Endelevu” yaani “AIDS is an unfinished Business.” Mkutano huu, Utatafuatiwa na mafunzo ya siku tatu wa Wakufunzi wa Rika “Peer Educators Training” yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusiana na masala ya UKIMWI na Afya katika maeneo ya kazi.

Hata hivyo Mafunzo hayo yamebeba kaulimbiu inayosema “Mafunzo kwa Waelimishaji Rika katika Maeneo ya Kazi ni Msingi Endelevu katika mapambano dhidi ya UKIMWI: Wakati ni sasa” yaani Workplace Peer Education is Key for Sustainability of HIV/Wellness Programs: Time to Act!”

Na vilevile Mkutano huo umehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkaazi wa UNAIDs, Dkt. Martin. Ordiit, Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI ( TACAIDs), Mwakilishi kutoka Ofisi ya Kamishna wa Kazi pamoja na wadau mbalimbali wa Masuala ya UKIMWI kutoka ndani na nje ya Nchi.

Post a Comment

0 Comments