Na Shemsa Mussa , Kagera.
Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Bukoba BUWASA imembaini Mwananchi mmoja wa kata ya migera Manispaa ya Bukoba kwa kujitahifisha huduma ya maji na kufanya shughuli za Umwagiliaji katika shamba lake la Vanila.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Bukoba BUWASA Bw Deogratius Sese wakati wa zoezi la ukaguzi wa bomba na vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na Mamlaka hiyo ili kutatua changamoto ya uhaba wa maji iliyokuwa ikiendelea katika maeneo hayo na ndipo walipogundua mteja wao Bw Noel Mtawa amekuwa akitumia maji kinyume na sheria.
" Tulipokea taarifa za kukosa maji kwa wakati na maeneo mengine kukosa kabisa katika maeneo haya ya magera mwisho wa rami na sisi kama BUWASA tukaja kuangalia maji yanapotelea wapi na nini tatizo ili tutatue wananchi wapate huduma ndipo tukakuta kuna huduma za umwagiliaji zinaendelea ndani ya uzio huu wa shamba la vanila.amesema Bw Sese"
Aidha Mkuregenzi huyo amesema kuwa zoezi hilo la ukaguzi wa bomba za maji nyumba kwa nyumba umekuja baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na wasamalia wema wakidai wamekuwa wakikosa maji kwa wakati na kumshuku( kuhisi)mtu huyo kufanya shughuli za umwagiliaji kila wakati katika shamba lake la vanila na amesema kuwa zoezi hilo la ukaguzi litaendelea ili kuwabaini waharibifu wengine wa miundombinu ya maji na baada ya hapo sheria itachukua nafasi yake.
"Tunawaomba wananchi msisite kutoa taarifa pindi mnapoona dalili zozote za uharibifu wa maji mkikaa kimya nyinyi,sisi kama serikali na nyie kwa pamoja tunapata hasara toa ishara na sisi tutafika na wala hatumtaji mtu na ukitoa taarifa sisi kama BUWASA tunatoa Bashasha kwa yeyote atakayefichuo uhovu kama huu ona sasa mpaka maji yametengeneza mfereji wa namna hii.ameongeza Bw Sese"
Hata hivyo Bw Sese amesema kuwa sheria namba 62 ya Mwaka 2019 imeweka wazi katika suala la Uharibifu wa miundombinu ya maji kuwa ikiwa mtu ataingilia miundombinu ya maji, uharibifu pamoja na wizi wa maji faini yake ni kiasi cha shilingi laki 5 hadi Milioni 50 ,kifungo cha miaka miwili hadi mitano au vyote kwa pamoja.
Naye Bi Jennifer Mtawa ambaye ni mke wa Noel Mtawa amekili kitendo hicho huku akisema kuwa kijana wake Denic Faida ambaye ni mfanyakazi katika shamba hilo la vanila ndiye alitoboa bomba hilo na kutengeneza mfereji kwa ajili ya maji kupita huku yeye hakujua na hakuwa na taarifa ya suala hilo.
0 Comments