***********
Na Shemsa Mussa, Kagera .
Mkurugenzi wa shule za kemebos na Kaizirege zilizopo katika halmashauri ya Bukoba Mkoani kagera Bw Eusto Kaizirege Ntagalinda ametimiza ahadi yake ya kutoa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita Mwaka 2023.
Awali akisoma lisara fupi Mkuu wa shule za kemebos na Kaizirege Mwl Kisha llamulila amesema kuwa wazo hilo la kutoa motisha ( tuzo) kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani yao ya taifa lililetwa Bw Kaizirege kwa lengo la kutoa hamasa kwa wanafunzi wazidishe juhudi kwenye masomo yao na tuzo hiyo ilipewa jina la(Eusto and Elizabeth Kaizirege Excellence Academic Award )
Zawadi hizo zilianza kwa kuwafadhili gharama za masomo kwa miaka miwili baada ya darasa la mitihani ikiwa wanafunzi waliofanya vizuri darasa la saba 7 ) walisoma bure kidato cha kwanza na cha pili na waliofanya vizuri kidato cha pili walisoma bure kidato cha tatu na nne huku waliofanya vizuri kidato cha nne walisoma bure kidato cha tano na sita.
Aidha Mwl Kisha ameongeza kuwa kwa matokea ya kidato cha sita yaliyotangazwa 13 Julai 2023 walipatikana washindi wawili waliopata dalaja la kwanza alama tatu (Division 1point 3 ) kwa kupata alama 'A' kwenye masomo matatu ya kwenye mchepuo wake .
Amewataja washindi hao wawili kuwa ni Janeth Byera Denis aliyekuwa akichukua mchepuo wa (ECA) unajumuhisha masomo ya Economics,Commerce na Accountancy na Shepherd Sabas Chambasi aliyekuwa akichukua mchepuo wa (PCM) unaojumuisha masomo ya Physics, Chemistry ,Advanced Mathematics huku wote wakipata division 1.3.
Pamoja na kujinyakulia kitita cha shiling Milion 5 kwa kila Mtu ikiwa kama pongezi kutoka kwa Mkurugenzi wa shule hiyo .
Hata hivyo baada ya kukabidhiwa hundi ya pesa wahitimu hao Janeth na shepherd wamesema kuwa siri ya mambo yote ni kumtanguliza Mungu kwa dua na sala, kutii nidhamu na kusoma kwa bilii pamoja na kujua na kutambua kwanini wapo shuleni.
Hafla fupi ya utoaji wa zawadi kwa wahitimu hao imefanyika katika viwanja wa shule hizo za kemebos na Kaizirege na kuhudhuliwa na wazazi wa wanafunzi hao wanafunzi , waalimu pamoja na viongozi wa dini.
0 Comments