Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI ULEGA, AWATAHADHALISHA WAFUGAJI WANAOFANYA MAENEO YA MALISHO KUWA VICHAKA.


Na Shemsa Mussa, Kagera.

Waziri wa Mifugo na uvuvi Mhe Abdallah Ulega awamepata tahadhali baadhi ya wafugaji wa ng'ombe wanaoyafanya malisho yao kuwa vichaka na mapori hatarishi kwa wananchi .

Ameyasema hayo wakati akifanya ziara ya kikazi ndani ya mkoa kagera na kuyambelea maeneo ya lanch, wafugaji wang'ombe pamoja na kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Kahama fresh kilichopo katika wilaya ya karagwe .


Amesema kuwa wapo baadhi ya wafugaji wanaomiliki maeneo makubwa bila ya kuyafanyia kile kilichokusudiwa na matokeo yake maeneo hayo hugeuka kuwa vichaka vikubwa na kuwa kero kwa wananchi.


"Sio kila mfugaji atatuletea maziwa wengine wataleta nyama ila lazima tuone hao ng'ombe wanaishi katika mazingira gani na sio unaomba eneo kubwa na mwisho wa siku unatuachia vichaka na migogoro isiyo isha hapo lazima tukunyanganye tu tuwape wenye uhitaji, amesema Mhe Ulega "


Aidha Mhe Ulega amesema serikali ya Dkt Samia imekuja na mfumo wa BBT ambapo kwa upande wa wizara ya Mifugo itakuwepo BBT live ya Maziwa na nyama itakayowahusisha vijana kwa lengo la kujikwamua kimaisha na kuwahasa wana kagera kuwa tayari kwa hilo.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Kahama fresh ltd Bw Jossam Ntangeki kinachozalisha Maziwa pamoja na uchakataji wa pamba na Alizeti amesema kwa sasa wanayo kampeini ya (kopa Ng'ombe lipa Maziwa) ambapoa mpaka sasa wamewafikia wananchi Mia 300 licha ya kuwepo changamoto ikiwemo uhaba wa eneo la malisho na uwepo wa wanyama waharibifu kama tembo wanaoharibu mazao na vyanzo vya maji.


Bw Jossam ameongeza kuwa kiwanda hicho mpaka kukamilika kitaghalimu kiasi cha shiling Bilion 8.6 na mpaka sasa kimefikia asilimia 90 na kusema kiwanda kitakapoanza kazi lasmi kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita elfu 20,000 kwa siku moja .

Post a Comment

0 Comments