Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Julai 10, 2023 Jijini Dar es Salaam amepokea vifaa vya michezo kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Chen Mingjian ambavyo vitatumika katika Programu ya Michezo Mtaa kwa Mtaa pamoja na Samia Taifa Cup.
Vifaa mbavyo Mhe. Chana amepokea ni pamoja na Mipira ya Kikapu 600, mipira ya Wavu 600, mipira ya Miguu 600 pamoja na Jezi 2634.
"Vifaa hivi tutavikabidhi katika mikoa yetu yote Tanzania Bara na Zanzibar bila kusahau Shule zetu mbili za michezo kwa kila Mkoa, naamini vifaa hivi vitanuafaisha vijana wetu katika kukuza vipaji ambavyo vitawasaidia wao binafsi na Taifa letu" amesema Mhe. Chana.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Chen Mingjian amesema nchi yake inaendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu wa wataalamu na ujenzi wa miundombinu ya michezo nchini.
0 Comments