Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI VINARA KWA KUANDIKA INSHA EAC NA SADC WAPEWA TUZO


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. James Mdoe,akikabidhi zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa tuzo kwa wanafunzi ambao ni washindi wa uandishi wa insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 huku ikisisitiza hamasa zaidi ili kupata washiriki wengi zaidi.

Akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo hizo leo Julai 15,2023 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. James Mdoe amesema kuwa uandishi wa insha ni sehemu ya mafunzo na inawajengea wigo mpana wa kujifunza masuala muhimu yanayohusu jumuiya hizo.

Prof.Mdoe amesema kuwa umuhimu wa kushiriki Mashindano hayo kwa wanafunzi ni kuwaongezea uwezo katika kukuza ujuzi wa lugha,unawaongezea maarifa kwa ujumla kwa kupata uelewa wa mada mbalimbali za masomo mengine na kuwasaidia kwa siku za usoni kunufaika na mtangamano wa Jumuiya hizo.

"Uandishi wa Insha unawapa wanafunzi fursa ya kutafiti na kupata taarifa zaidi, kuelewa na kuwawezesha kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na Jumuiya zetu na husaidia wanafunzi wa Kitanzania kuchanganua masuala kutoka nyanya mbalimbali na kulinganisha nyanja hizo na Mazingira yetu," amesema Prof Mdoe.

Hata hivyo amewapongeza wanafunzi wote walioshiriki katika shindano hilo tangu ngazi za awali na kubainisha kuwa licha ya changamoto ndogo ndogo zilizopo katika sekta ya elimu lakini ubora wa elimu ni mzuri na hilo linadhihilishwa kwa wanafunzi wengi kuonyesha ushindani mkubwa katika uandishi wa insha ikishirikisha nchi mbalimbali.

Ameongeza kuwa “Ni matamanio yetu siku moja tuone washindi wa kwanza, wa pili, wa tatu hata hadi nafasi ya tano tunakuwa watanzania na hili linawezekana tukitilia mkazo walimu wakuu, wazazi na waratibu wahamasishe zaidi” amesema Prof. Mdoe.

Aidha Prof. Mdoe amewataka Walimu Wakuu na Waratibu wa ndani wa Shule mbalimbali nchini kuhakikisha wanawasaidia wanafunzi wao miongozo inayohitajika katika uandishi wa Insha.

Awali, akisoma risala ya mashindano hayo, Mratibu wa Insha kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bi.Matuha Masati,ameipongeza Sekretarieti ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Nchi za SADC Kwa kuendesha Mashindano ya Uandishi wa Insha kwani yamekuwa chachu Kwa vijana kufanya utafiti,kujifunza na kufahamu vizuri mchakato na hatua mbalimbali za uimarishaji Kwa nchi wanachama.

Amesema kuwa mashindano hayo husimamiwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) kwa insha za nchi za Afrika Mashariki (EAC) na za SADC husimamiwa na Wizara ya Elimu kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar.

Amesema kuwa Jumla ya wanafunzi 133 walishiriki katika shindano la uandishi wa Insha za SADC Kwa Mwaka 2021 na baada ya usahihishaji wakapatikana washindi 10 katika ngazi ya Taifa ambao wamepewa zawadi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwa ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo zawadi zilikuwa zikitolewa Kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu tu

" Kwa upande wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki washiriki walikuwa 315 Kwa Mwaka wa 2021 ambapo baada ya usahihishaji wakapatikana washindi 10 ambao wamegawanywa katika Makundi mawili” amesema.

Ameongeza kuwa "Kundi A wanapewa zawadi tofauti tofauti kulingana na nafasi ya ushindi kitaifa na kundi B ni mshindi kuanzia nafasi ya Sita hadi kumi hawa wanapewa zawadi zinazofanana kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,"amefafanua Masati

Katika mashindano ya SADC mshindi wa kwanza amepata Dola za Marekani 500, wa pili amepata Dola za Marekani 300 na watatu amepata Dola za Marekani 200 huku kwa EAC mshindi wa kwanza amepata Dola za Marekani 300, wa pili Dola za Marekani 250 na watatu amepata Dola za Marekani 200 , wan ne amepata Dola za Marekani 150 na watano amepata Dola za Marekani 100.

Aidha, katika kundi la pili kwa EAC lilikuwa na wanafunzi watano ambao kila mmoja amepata Dola za Marekani 50 na Wizara imetoa Sh. 300,000 kwa washindi 20 wa mashindano hayo.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akizungumza wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.


Mratibu wa Insha wa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bi. Matuha Massati, akisoma risala wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe,akipokea risala kutoka kwa Mratibu wa Insha wa Wizara hiyo Bi. Matuha Massati,wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.




Mwakilishi wa Katibu Mkuu TAMISEMI, Alfred Kazimoto,akizungumza wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. James Mdoe (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. James Mdoe,akikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.


Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Zanzibar Bi.Asya Idd Issa ,akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.


Mratibu NECTA Dodoma Bw.Ezekiel Sekelano,akizungumza wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.


Mratibu wa Insha Shule ya Sekondari Azania Mwalimu Ndeni Ndossi,akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kutunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. James Mdoe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwatunuku zawadi kwa washindi wa Kitaifa wa Shindano la Uandishi wa Insha kwa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2021 hafla iliyofanyika leo Julai 15,2023 jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments