Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI WA HOTELINI 700 MKOANI ARUSHA KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA UJUZI

Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Robert Masingiri,akifungua Julai 24, 2023 mafunzo ya wiki moja ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 700 wa mkoani Arusha.

Wafanyakazi wa hotelini mbalimbali wakishiriki mafunzo ya kukuza ujuzi yanayofanyika mkoani Arusha Julai 24 hadi 29, 2023.


Mwezeshaji wa masuala ya huduma na chakula hotelini Richard Makori akitoa elimu kwa wafanyakazi wa hotelini kwenye mafunzo ya kukuza ujuzi yanayofanyika mkoani Arusha Julai 24 hadi 29, 2023.


Mwezeshaji wa masuala ya huduma ya mapokezi hotelini Jovita Costas akitoa elimu kwa wafanyakazi wa hotelini kwenye mafunzo ya kukuza ujuzi yanayofanyika mkoani Arusha Julai 24 hadi 29, 2023.


Mwezeshaji wa masuala ya mapishi Fransis Makori akitoa elimu kwa wafanyakazi wa hotelini kwenye mafunzo ya kukuza ujuzi yanayofanyika mkoani Arusha Julai 24 hadi 29, 2023.


Mwezeshaji wa masuala ya usafi hotelini Jane Tarimo akitoa elimu kwa wafanyakazi wa hotelini kwenye mafunzo ya kukuza ujuzi yanayofanyika mkoani Arusha Julai 24 hadi 29, 2023.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza kutoa mafunzo ya kukuza ujuzi kwa wafanyakazi wa hotelini 700 mkoani Arusha ili kuwa na weledi wa kuhudumia watalii wanaokuja nchini.

Mafunzo hayo yanatolewa kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi iliyopo chini ya ofisi hiyo ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kupaisha sekta ya utalii nchini kwa kuhakikisha watalii wanahudumiwa kwa weledi na ujuzi stahiki.

Akifungua mafunzo hayo Julai 24, 2023 jijini Arusha, Mkurugenzi Msaidizi wa Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi hiyo, Robert Masingiri, amesema mafunzo hayo ni ya wiki moja na yamegusa idara zote za hotelini ili watalii wanaokuja wapate huduma bora.

“Lengo la serikali pamoja na elimu mliyonayo inawaongezea ujuzi zaidi wa kuhudumia hawa wageni wetu ili kuvutia wengi zaidi kuja nchini na kufikia idadi ya watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025,”amesema.

Amewahimiza washiriki kuzingatia mafunzo hayo ambayo yamebeba ujuzi wa maeneo mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments