Ticker

6/recent/ticker-posts

VETA MKOA WA SHINYANGA NA DODOMA WAONESHA UMAHIRI WAO KWENYE USUSI NA UREMBO

Katika kukabiliana na wimbi la ajira nchini vyuo vya VETA katika Mikoa ya Shinyanga na Dodoma, Dar es Salaam pamoja na Iringa zimeona mafunzo ya ususi na urembo ni moja fursa ya kuwakwamua vijana kwenye ajira.

Ususi na Urembo ni fursa ya kutoa ajira kwa vijana kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa katika urembo wa ususi.

Akizungumza kwenye Banda la VETA katika Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam. Dar es Salaam, Mwalimu wa Ususi na Urembo VETA Dodoma, Hamisa Amir amesema wanatoa mafunzo ya ususi na urembo kuanzia umri wa miaka 18-35 kwa vijana ambao hawajui kabisa na wenye ujuzi miaka 18 na kuendelea.

Mafunzo ya urembo mara nyingi hufanywa na wanawake lakini hata wanaume wanaweza kujifunza nao wakawa wanafanya kazi za urembo.

Mafunzo ya urembo hayachagui Jinsia hivyo kila kijana anaweza kujifunza kutokana na kuwepo kwa soko kubwa ya wahitaji wa urembo.

Amesema kuna baadhi ya nchi wanaume ndio wanaendesha ofisi za urembo kwa kushiriki wenyewe ikiwemo nchi ya Demokrasia ya Kongo.

Amesema sekta ya urembo inakua kwa kasi kwa sababu wanaosoma fani hiyo wameongezeka ikiwa tofauti na miaka ya nyuma na wanaangalia mitindo inayoendana na soko la duniani.

“Mafunzo hayo tunatoa shinyanga, Dodoma, Iringa, Dar es Salaam na mikoa mingine tuna malengo makubwa na kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia sekta hii na tunatoa mafunzo ya wiki moja,” amesema Hamisa.

Amesema mafunzo hayo wanatoa juu ya namna bora ya kupata elimu ya matumizi ya vifaa kuepusha madhara kwa wateja kutokana na matumizi ya vifaa hivyo.

Hamisa amesema asilimia 99 ya vijana wengi fani hii wanajifunza mtaani hivyo ni vigumu kupata ajira.

Aidha amesema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni vijana wengi kutokuwa na elimu ya Ususi na urembo wanao hudumia wengi hawana taaluma.

“Vijana wa kiume wanasoma fani hii ni wachache wanakuwepo wawili hadi watano wengi wanajifunza mtaani ambao hawana ujuzi inasababisha kuharibu nywele za wateja kutokana na kukosa elimu ya kazi hiyo. mteja,”amesema.


Mwalimu wa Fani ya Ususi na Urembo wa Chuo cha VETA Dodoma Hamisa Amir akionesha umahiri wa kusuka kwa Mteja aliyetembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments