Ticker

6/recent/ticker-posts

SHEHENA YA MIZIGO YAPAA BANDARI YA TANGA

Takwimu za ongezeko la shehena za Mizigo katika bandari ya Tanga kwenda maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi zimeripotiwa kuongezeka kwa asilimia 8.2 ikiwa ni ongezeko ndani ya miezi 6 kwa mwaka 2023.

Akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Kamati ya Maboresho ya Huduma za Bandari kwa bandari ya Tanga mkoani humo, Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Aron Kisaka amesema Serikali inategemea ongezeko zaidi baada ya maboresho yaliyofanyika hivyo Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inapashwa kuhakikisha kitengo cha masoko kinajipanga.

“Baada ya uwekezaji kwenye Miundombinu hususani gati na vitendea kazi tutegemee mzigo mwingi zaidi hivyo ni wajibu wa idara ya masoko kuhakikisha mazigo unahudumiwa vizuri ili kufanya wateja wasihame bandari ya Tanga’ amesema Mhandisi Kisaka.

Mha Kisaka ameitaka TPA kuhakikisha inaogeza kasi kwenye mazungumzo na makampuni mengine ya meli ili kuhakikisha idadi ya mzigo inaongezeka na hatimaye uwekezaji kuwa kuwa na tija kwa Serikali na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Peter Milanzi amesema Serikali kupitia TPA kwa mwaka 2023/24 imejipanga kuongeza gati mpya mbili kwa kutenganisha gati kwa abiria na mizigo ili kurahisisha shughuli za uchukuzi katika bandari hiyo.

Naye mdau wa Bandari nchini Bi Lilian Mbwambo kutoka Kampuni ya Uwakala wa Meli ya Tanga Modern amesema Utaratibu wa Serikali wa kuwa na vikao vya pamoja na wadau wote kutarahisha kutatua changamoto zilizopo kwa wakati ili kurahisisha usafirishaji katika bandari hiyo.

Serikali kupitia TPA imekuwa ikiendesha vinavyowakutanisha wadau wote wanaoshughulia na bandari kwa lenngo la kutatua changamoto mbalimbali za uendeshaji kwa pamoja.


Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Aron Kisaka akisisitiza jambo kwa wadau mbalimbali wa huduma za Bandari Nchini (hawapo pichani) wakati akifungua mkutano wa kamati ya maboresho ya huduma za bandari kwa bandari ya Tanga, Mkoani humo.
Baadhi ya Wadau mbalimbali wa huduma za Bandari Nchini wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi Mha Aron Kisaka (hayupo pichani) wakati alipofungua mkutano wa kamati ya maboresho ya huduma za bandari kwa bandari ya Tanga, Mkoani humo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Peter Milanzi akitoa ufafanuzi katika kikao cha toa hoja kwa wadau wa Bandari Nchini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kamati ya maboresho ya huduma za bandari kwa bandari ya Tanga kilichofanyika Tarehe 10 Julai,2023 Mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments