Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeendelea kutoa uelewa wa masuala ya utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia kwa wananchi na makundi mbalimbali ya wadau wanaotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 47 ya Saba Saba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kutoa elimu hiyo, PURA pia inaelezea majukumu inayoyatekeleza kwa mjibu wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 yakiwemo kuishauri Serikali juu ya masuala ya mkondo wa juu wa petroli; kusimamia na kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli; na kuhamasisha ushiriki wa Watanzania katika miradi ya mafuta na gesi asilia inayotekelezwa nchini.

Bw. Hakeem Mwaruka kutoka PURA akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika banda la PURA katika maonesho ya 47 ya Saba Saba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.


0 Comments