Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) Gabriel Migire amelitaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Zanzibar ili kuhakikisha reli itakayojengwa visiwani humo inakuwa na viwango na kukidhi matarajio.
Reli hiyo inayotarajiwa kujengwa katika maeneo ya Bububu, Mangapwani, Makobe, Bandaa kuu, Matemwe, Pwani, Mchangani, Kiwengwa hadi Pongwe ina lengo la kurahisisha shughuli za uchukuzi wa abiria na mizigo na utalii kutoka bandarini kuelekea maeneo mbalimbali ya mji.
Akizungumza jijini Arusha wakati akifunga Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa Sekta ya Uchukuzi na taasisi zake kutoka Tanzania Bara na Viongozi na Wataalam wa Wizara hiyo kutoka Visiwani Zanzibar Katibu Mkuu Migire amesema malengo yaviako vya kubadilisha uzoefu ni pamoja na kushirkiana katika utekelezaji, usimamizi na uendeshaji wa miradi ya Usafirishaji.
“Ni kweli kutokana na ongezeko la watu katika Visiwa vya Zanzibar wizara ujenzi na Uchukuzi kutoka Tanzania Bara na kutoka Zanzibar zinapashwa kushirikiana ili kuakikisha changamoto za usafirishaji zinapata muarobaini ili kuchagiza zaidi shughuli za usafirishaji” amesema Migire.
Katibu Mkuu Migire ameongeza kuwa Miradi yote ya Serikali ya Tanzania Bara na Visiwani inayotekelezwa ikikamilika kwa viwango na ubora itachangia urahisi wa bei ya usafiri kushuka lakini pia bei ya bidhaa kuwa rafiki kwa watumiaji.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kutoka Zanzibar Shomari Omari Shomari ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiti TRC kwani kupitia uzoefu wao wa ujenzi na uendeshaji war lei utaisaidia Wizara hiyo kusimamia na kuendesha miradi hiyo k wa ufanisi.
“Pamoja na kutokuwa na Shirika linalosimamia na kuendesha Reli visiwani kwetu tumeanza maandalizi ya ujenzi wa reli na tunaimani ushirkiano tutakaoupata kupitia TRC utatusaidia zaidi kwenye ujenzi na uendeshaji” amesema Naibu Katibu Mkuu Shomari.
Kwa upande wa Usafiri wa Anga Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi amesema Serikali kupitia Air Tanzania iko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taratibu ili kuanzisha safari za ndege kutokea Dar es Salaam kwenda Unguja na Pemba.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa zikiwakutanisha viongozi na watalaam wa hizo mara nne kwa mwaka kwa lengo la kupeana uzoefu katika uendeshaji wa sekta ndogo za Usafiri kwa Njia ya Maji, Anga, Reli na Bandari.
Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Sekta ya Uchukuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mara baada ya kufunga kikao cha Mashirikiano kilichowakutanisha Wizara hizo mbili jijini Arusha Mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Sekta ya Uchukuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, taasisi zilizo chini ya Wizara hizo na wataalaam mara baada ya kufunga kikao cha Mashirikiano kilichowakutanisha Wizara hizo mbili jijini Arusha Mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Sekta ya Uchukuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wataalaam kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mara baada ya kufunga kikao cha Mashirikiano kilichowakutanisha Wizara hizo mbili jijini Arusha Mwishoni mwa wiki.
0 Comments