Na Shemsa Mussa, BUKOBA, KAGERA.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Fatma Mwassa amewasili Mkoani Kagera baada ya kukamilisha nguzo moja wapo ya uislam alipokwenda Hijja katika Mji wa Makha Nchini Saudi Arabia huku akiwabebea Wana Kagera na Watanzania zawadi ya Dua pamoja na maono yenye kuwafanya kuamini kuwa tayari wamesamehewa makosa yao kupitia maombi aliyoyafanya katika ibada hiyo.
Akizungumza baada ya mapokezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege Manispaa ya Bukoba Fatma Mwassa amesema kuwa anayekwenda kuhiji akifanya Hijja ya kweli na kurudi salama lazima pawepo na mabadiliko ikiwa ni pamoja na mfumo wake wa maisha ,kuongeza nguvu katika kumcha Mungu, unyenyekevu na hofu ya Mungu.
Aidha ameyataja mambo makuu aliyoyaweka katika ibada hiyo kwa Watanzania na WanaKagera kuwa ni pamoja na kuwepo na uongozi wenye maelewano Masikilizano , Roho ya ushindi na yenye kutokata tamaa, kuondokana na malalamiko, ujasili wa kuamini kushinda na kuwepo mzunguko wa fedha na kupata mali.
" Nilipo simama Arafa niliomba sana na kuliombea taifa langu na hasa wana karega naamini niliyoyaomba yoote yatajibiwa na tutafanya kazi kwa amani na kwa baraka za Mungu .amesema mh Fatma "
Alitumia nafasi hiyo kuwaomba Wananchi Mkoani humo kila mtu kwa imani yake na kwa dini yake kuendelee kumcha Mwenyezi Mungu na kuwa na hofu nyikwa kwa Mungu .
" Najua hapa kagera tunaamini sana Mungu na tuendelee hivyo kila mtu na imani na dini yake tutafika mbali sana na kwa Muda mfupi sasa mmeshampata Mkuu wa Mkoa Hajat mimi ni Hajat jamani.Ameongeza Hajat Fatma "
Mkuu huyo wa Mkoa amemaliza kwa kuwapatia zawadi ya dua wana kagera na kufanya zoezi la komba kwa pamoja .
0 Comments