Ticker

6/recent/ticker-posts

MILANGO YA MAKUMBUSHO IPO WAZI KWA WANAOTAKA KUANZISHA MAKUMBUSHO BINAFSI

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi yake ya Makumbusho ya Taifa, imejipanga vyema katika Uhifadhi wa Makumbusho na Malikale Ili rasilimali hizo adhimu za Kihistoria ziweze kuinufaisha jamii ya Sasa na vizazi vijacho.

Hayo yamese na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga alipotembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya kimataifa Jijini Dar es Salaam, ili kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali zinzofanywa na Taasisi na Idara za Wizara hiyo.

Dkt. Lwoga amesema kuwa, Taasisi ya Makumbusho ya Taifa itaendelea kushirikiana na Taasisi na Idara zote za Wizara hiyo kwa minajili ya Uhifadhi endelevu wa Malikale, uboreshaji wa vituo vya Makumbusho pamoja na uwanzishwaji wa Makumbusho mpya.

Licha ya kuzungumzia Shughuli zinazofanywa na Taasisi yake ambazo ni pamoja na Uhifadhi, Utafiti, Ushauri na Uelimishaji kupitia maonesho mbalimbali yaliyomo kwenye vituo vya Makumbusho nchini, ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana na Taasisi hiyo.

Dkt Lwoga amesema kuwa Makumbusho ya Taifa imejipanga vyema kuhudumia taasisi, mashirika na watu binafsi wanaotaka kuanzisha Makumbusho binafsi.

Aidha Dkt. Lwoga amezipongeza Taasisi na Idara zinazoshiriki Maonesho hayo Makubwa ya Kimataifa, kwa namna zilivyo jiandaa vyema katika kuujuza umma juu ya matokeo chanya ya Utekelezaji wa Shughuli za Wizara hasa katika Uhifadhi na Utangazaji ili kuvutia Watalii wengi zaidi nchini na kuinua Pato la Taifa.

Post a Comment

0 Comments