MBUNGE wa Jimbo Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Taasisi ya Tanga Yetu kupitia ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation katika Jiji la Tanga kushoto ni Mwakilishi wa Botnar Tanzania Dkt. Hassan Mshinda
MBUNGE wa Jimbo Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Taasisi ya Tanga Yetu kupitia ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation katika Jiji la Tanga kushoto ni Mwakilishi wa Botnar Tanzania Dkt. Hassan Mshinda
MKURUGENZI wa Kampuni ya V.J Mistry& Co.Ltd inayojenga Forodhani ya Tanga Jitesh Jethwa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa ziara hiyo
MKURUGENZI wa Kampuni ya V.J Mistry& Co.Ltd inayojenga Forodhani ya Tanga Jitesh Jethwa kulia akimuonyesha maeneo mbalimbali Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa ziara hiyo
Na Oscar Assenga, TANGA
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema kuwa kupitia fursa ya uchumi wa bluu wananchi wa Jiji la Tanga wataweza kujiongezea fursa ya shughuli za kiuchumi ikiwemo kujiongezea kipato kupitia fursa za ufugaji na kilimo kupitia bahari.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya aliyasema hayo wakati alipotembelea miradi inayotekelezwa na Taasisi ya Tanga Yetu kupitia ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation katika Jiji la Tanga huku akiwashukuru kwa kukubali ombi lake kutekelezwa miradi hiyo ambayo itasaidia kukuza uchumi wa bluu.
Miradi hiyo ni ya uvuvi, kilimo cha mwani, jongoo bahari na unenepeshaji wa kaa pamoja na ufugaji wa samaki, kuku na kilimo cha mbogamboga katika kata za Tongoni, masiwani, Tangasisi, Usagara na Central.
Aidha Botnar foundation pia wamefadhili miradi ya Afya, Elimu na kujenga Forodhani ya Tanga.
Katika miradi hiyo jumla ya fedha zilizotumika hadi sasa ni kiasi cha shilingi bilioni 5.65 zimetumika ambayo kwa asilimia kubwa zimewasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.
Alisema kutokana na umuhimu wa uchumi wa bluu katika kukuza uchumi wa wananachi hivyo Jiji hilo limejipanga kuwa kinara katika uzalishaji wa majongo bahari, unenepeshaji wa kaa pamoja na kilimo cha mwani kwa kutumia fursa ya bahari iliyopo kwenye Ukanda wa Pwani.
Alisema kwa sababu mkoa wa Tanga una eneo kubwa la bahari na tayari mafanikio yamekwisha kuyaona hivyo tumejipanga kuongeza uzalishaji Ili tuweze kuwa vinara wa kutumia fursa za uchumi wa buluu Kwa maendeleo ya watu wetu sambamba na nchi kupata mapato yake”amesema Waziri Ummy.
Alisema kutokana na uwepo wa fursa wanapaswa kulikumbatia zao la mwani kwa sababu ni zao ambalo kilimo chake sio kigumu zaidi na faida yake ni kubwa.
“Mimi kama Mbunge wa Jimbo la Tanga nitashirikiana na wadau Botnar Foundation kuendeleza kilimo cha mwani kikubwa tuwape elimu na ujuzi wananchi hususani wanawake ikiwemo kuwapa vitendea kazi ambayo vitasaidiaa kufanya vizuri katika kilimo cha Mwani na kutafuta masoko”Alisema Mbunge Ummy.
Aidha alisema kwamba amejipa kazi maalumu ya kutangaza mazao makubwa matatu Tanga mjini kutokana na kwamba wanataka mwambao wa Tanga uwe maarufu kwa kuzalisha mazao ya Mwani,Majongoo Bahari na kunenepesha kaa.
Alisema kwamba hayo mazao matatu amevutiwa nayo na kama watawekeza kwenye uchumi wa bluu utasaidia watu wengi sana kupata kipato na hivyo kuweza kujikwamua kiuchumi.
“Lakini niwahaidi kwamba nitafatuta kiwanda cha mwani ili wakiweke kwenye Jiji la Tanga hivyo niwahamasishe watu wengi walime mwani na nimewaomba botnar watusaidie hivyo wananchi tusikate tamaa mapema mwani utalipa hivyo tujitume kulima”Alisema Mbunge Ummy
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwakilishi wa Botnar Tanzania Dkt. Hassan Mshinda amemuhakikishia Mbunge Ummy kuwa Botnar itaendelea kushirikiana nae na Halmashauri ya Jiji la Tanga katika kutatua kero za maendeleo kwa wakazi wa Tanga Mjini hususan vijana na watoto.
0 Comments