Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE LUCY MAYENGA ASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO KWA MAVETERANI


Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akiwashangilia Maveterani
Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga (aliyevaa miwani) akiwashangilia Maveterani


Na Mwandishi wetu - Kishapu

Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga ameshiriki katika fainali ya bonanza la michezo kwa Maveterani wa timu mbalimbali lililofanyika wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.


Bonanza hilo lililohitimishwa Julai 9,2023 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi lililenga kuhitimisha sherehe za Sabasaba liliandaliwa na Maveterani wa wilaya ya Kishapu.

Timu za Maveterani zilizoshiriki ni pamoja na timu kutoka Shinyanga, Kakola, Kagongwa, Simiyu, Tabora, Musoma na timu mwenyeji ya Kishapu ambapo timu za Kishapu na Shinyanga zilifanikiwa kutinga fainali na Kishapu kufanikiwa kutwaa kombe.


Mbunge huyo wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga amekuwa mdau na sehemu ya udhamini wa bonanza hilo liliofanyika siku mbili kuanzia tarehe 08-09/7/2023.


Katika kukabidhi kombe na medali kwa washindi ambao ni Kishapu Veterani Mhe. Mayenga alitoa pia shilingi 100,000/= kwa mshindi wa pili ambaye ni Shinyanga Veterani.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika bonanza hilo Mhe. Lucy Mayenga alitumia nafasi hiyo kutoa jezi, mpira na 50,000 kwa timu ya Talent FC (timu ya Mhunze) ambayo iliwasilisha ombi hilo kwake siku ya tarehe 04/07/2023.

Mhe. Mayenga aliwashukuru wananchi, Mbunge wa jimbo Mhe. Boniphace Butondo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi na waaandaji kwa tukio hilo zuri lenye kuleta mshikamano.

Akikabidhi kikombe cha ushindi kwa mshindi wa Bonanza hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi alisema michezo ni afya, inaleta umoja na mshikamano huku akihimiza jamii ya wana Shinyanga kuipenda michezo ili kuleta mshikamano.
Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akiwashangilia Maveterani (aliyevaa miwani) akifuatilia michezo ya Maveterani
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga, Grace Bizulu akiteta jambo na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mh. Lucy Mayenga

Post a Comment

0 Comments