Ticker

6/recent/ticker-posts

MAABARA YA NELSON MANDELA YAPONGEZWA


Mkuu wa Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Bw. Omari Issa akiongea na menejimenti ya chuo (hawapo katika picha) jana tarehe 27 Julai ,2023 wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa chuoni hapo tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mkuu wa Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Bw. Omari Issa (Kulia) akisisitiza jambo alipotembelea mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wasiopungua 500 amabo utakuwa na vyumba 42 maalum kwa ajili ya wakina mama wenye watoto wadogo wakati wa ziara yake ya siku mbili , katikati ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Professa Lughano Kusiluka na kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo Fedha, Mipango na Utawala Profesa Suzana Augustino.


Mkuu wa Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Bw. Omari Issa (kulia) akipata maelezo kuhusu shughuli za Maktaba kutoka kwa Mkurugenzi wa Maktaba Dkt. Neema Mosha (kushoto) wakati wa ziara yake ya siku mbili


Mkuu wa Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Bw. Omari Issa (katikati) akipata maelezo kuhusu shughuli za Maabara kutoka kwa Mkuu wa Maabara Dkt. Ramadhani Sinde (kulia) wakati wa ziara yake ya siku mbili


Mkuu wa Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Bw. Omari Issa (kulia) akipata maelezo kuhusu bidhaa za ngozi zinazotengenezwa kwa ubunifu wa dawa ya asili ya kusindika ngozi kutoka kwa Mbunifu na Mhadhiri wa Chuo hicho Dkt. Cecilia China (Katikati) wakati wa ziara yake ya siku mbili

Na.Mwandishi Wetu-ARUMERU

Mkuu wa Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Bw. Omari Issa amekipongeza chuo hicho kwa kuwa na Maabara ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kufanya vipimo mbalimbali na kuja na majibu chanya kwa maendeleo ya nchi.

Bw. Omari ameyasema hayo katika Kampusi ya chuo hicho kilichopo Wilaya ya Arumeru Tengeru Jijini Arusha akiwa anahitimisha ziara ya siku mbili aliyoianza tarehe 26 Julai, 2023 kwa lengo la kutembelea taasisi hiyo tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 6 Juni, 2023.



"Maabara hii ni kubwa na ya kisasa yenye ina uwezo mkubwa wa kupima vitu mbalimbali nami naahidi ntakutana na viongozi wenzangu ili kuangalia namna ya kuitumia maabara hii katika kupata majibu ya vipimo mbambali ikiwemo kufanya kazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali" alisema Bw. Omari Issa



Aidha, Bw. Omari alitoa maagizo kwa wasimamizi wa Maktaba katika chuo hicho kuhakikisha tafiti na bunifu mbalimbali zinazotolewa zinaingizwa kwenye kompyuta ili vyuo vingine vya ndani na nje viweze kupata uwelewa zaidi kuhusu Nelson Mandela.



"Lazima tafiti zinazofanywa hapa zilete fursa ya biashara na hivyo kusaidia katika kutimiza malengo ya chuo" alisema Bw. Omari Issa



Vilevile alitoa rai kwa watafiti wanaofanya tafiti katika vyuo mbalimbali kushirikiana zaidi katika sekta hiyo ili kuondokana na tafiti zinazojirudia pale zinapotangazwa.



Bw. Omari aliiagiza Shule ya Biashara na Insinia (BuSH) pamoja na Shule ya Nishati Malighafi, Nishati Maji na Sayansi ya Mazingira (MEWES) kuandaa andiko litakalosaidia kutatua changamoto ya nishati mbadala.



Kwa upande wa uongozi Bw. Omari Issa alisisitiza umuhimu wa mafunzo kwa viongozi na wafanyakazi ili kuwa na mfumo mzuri wa utekelezaji wa majukumu ya kila siku.



“kitu kikubwa ambacho kitatusaidia kusonga mbele na kuleta mabadiliko sisi kama jumuiya ya Nelson Mandela ni uadilifu, akili, nguvu na kufanya kazi kwa umoja" amesema Bw. Omari Issa



Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Professa Lughano Kusiluka ameahidi kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Mkuu huyo wa Chuo kwa kutoa tafiti zenye tija ikiwemo kuzalisha wabunifu mbalimbali ambao watatumia chuo hicho kwa ajili ya kufanya biashara na kujikwamua kimaendeleo.

Post a Comment

0 Comments