Ticker

6/recent/ticker-posts

DC MWEGELO AFAFANUA MAAMUZI MAGUMU YA RAIS SAMIA UWEKEZAJI BANDARI

Na Hamida Kamchalla, KOROGWE.

HATUA iliyofikiwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kwenda kinyume na utendaji wa mazoea na kufanya maamuzi magumu katika uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam imetajwa kuwa ni mwarobaini wa kujirudia mara kwa mara kwa taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (CAG).

Akizungumza kwenye mkurano maalumu kwa ajili ya ujio wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) Daniel Chongolo, mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo amesema hatua hiyo ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan siyo kitu rahisi kwakuwa ameachana na mazoea yaliyozoeleka na watu kwani ilikuwa ni tiamaji tiamaji kutokana na taarifa ya CAG masuala yanayoibuliwa ni yaleyale lakini mwarobaini haukuwahi kupatikana.

"Sasa kwa utashi wake pamoja na ushauri alioupata, wakasema lazima tuimarishe bandari na miundombinu yetu, lakini uendeshaji wake uendane na mahitaji ya kileo na utusaidie Tanzania kukaa kimkakati" amesema Mwegelo.

Aidha amebainisha kwamba kwenye midahalo mingi, serikali ya Tz inasomeka kama ni nchi kubwa ambayo imelala hivyo Rais Samia Suluhu Hassan amekataa hali hiyo na kuamua kama serikali kwani nchi ina rasilimali za kutosha kusimama na kujiendesha.

"Sisi watu wa midahalo, ukienda kwenye midahalo mingi Tz tunasomeka kama (sleeping Giant) yaani jitu fulani kubwa ambalo limelele tu, tafsiri nyepesi ni kwamba tuna rasilimali za kutosha, tuna uwezo mkubwa, uwezo wa uchumi wetu Barani Afrika ni mkubwa, lakini tumeendeleza nadharia hatujaenda kwenye uhalisia" amesema.

"Wakati natumikia Dar es salaam, nikienda kule bandarini nakuta magari mengi ya mizigo yasiyopungua 8, lakini yanaenda nje ya nchi na hayo ni magari tu, kwahiyo tunaona ni kiasi gani kama nchi tukiamua kujisimamia vizuri, yule aliyetuita jitu lililolala, anakuta yuko macho na anavuruga kuchanja mbuga na kufikia malengo yake" amesisitiza.


Mkuu huyo amefafanua kwamba hiyo imemfanya Rais Samia Suluhu Hassan kukataa jina hilo katika uongozi wake wa serikali ya awamu ya sita na kwamba ingawa maamuzi hayo ni magumu na wapo watu wengi ambao wanayapinga na kutaka kufanya ilivyozoeleka kwa kutumia nafasi na taaluma zao kwa maslahi yao binafsi lakini mchakato wa jbo hilo umepitiwa na kudhiriwa na Bunge lakini pia kwenye halmashauri kuu ya Ccm Taifa.


"Ninyi wengi ni mashahidi, ukifanya maamuzi magumu siyo, kwa hili watatokea watu, watatumia nafasi na taaluma zao kupotosha, kwasababu pennine wana maslahi yao binafsi, lakini mimi naamini na ninawaomba na ninyi twende na imani hiyo,


"Kwasababu Mh. Rais alifanya jambo hili na likapitishwa na Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tz, lakini halikuishia hapo akalipeleka kwenye halmashauri kuu ya Ccm Taifa, wakawasilishiwa taarifa, wakapitia, wakachambua na wakaridhia, na katika maadhimio ni kwamba jambo hili linalotaka kufanywa na serikali ya awamu ya 6 ni jema na liendelee" amebainisha.


Hata hivyo Mwegelo kwa upande wa Bandari ya Tanga, wamejiwekea mpango mkakati katika Wilaya ya Korogwe kwa kuongea na wawekezaji ili kuona namna ya kuitumia bandari hiyo kupitishia mizigo yao kwani itasaidia sana kupunguza garama kwa kutumia bandari ya Dar es salaam.


"Tulitoka hapa na watu sio chini ya 70 tukatembelea bandari yetu ya Tanga ambayo Rais wetu amewekeza mamilioni ya fedha kuiboresha ili iweze kubeba mizigo ya kutosha, na uboreshaji huu utapunguza garama ya kupeleka mizigo katika bandari ya Dar es salaam,


"Na tukipunguza garama, bei za bidhaa zetu zitakua za ushindani zaidi na sisi hapa Korogwe tuna mazai mbalimbali kama chai, mkonge lakini pia tuna mazao ya chakula ambayo ni ya biashara" amebainisha mkuu huyo wa Wilaya.


Kwa upande wao, mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji na Mkuu wa wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando wakiwa kwenye mkutano huo wamesema uwekezaji umetokana na makusanyo ya bandari ya Daresalaam na kufanya viongozi wakuu wa nchi kuona umuhimu wa kutafuta mwekezaji.


"Bandari kwetu imekuwa ndio langu kuu la kiuchumi hasa bandari ya Daresalaam, Tanga na nyinginezo tukiangalia historia kidogo bandari zetu hazifanyi kazi vizuri na hazina mafanikio sana ni kwanini hali hii ndio imepelekea mheshimiwa Rais pamoja na watawala wake na baraza la mawaziri kuamua kutafuta mwekezaji, "meisema Kaji.


"Wale ambao wanajaribu kupotosha au kusema tofauti kwanza watambue hii sio ligi ya kushindana nani anajua kusema sana na nani hajui tunachokifanya sisi ni kuzungumzia au kusema mustakabali wa nchi yetu maslahi ya nchi yetu na nini watanzania wanakitaka kutoka kwetu sisi ambao tumepewa dhamana ya uongozi, "amesema Wakili Msando.


Hatua ya Mkutano huo imekuja mara baada ya kuwepo kwa taarifa tofauti dhidi ya uwekezaji huo huku serikali ikisema hatua hiyo itasaidia kuongeza ufanisi kwenye bandari ya Daresalaam na kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa.


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) Daniel Chongolo kesho anatarajiwa kuhutubia maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Tanga katika mkutano utakaofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mazoezi akiongozana na wataalamu wabobezi wa masuala ya uwekezaji mahali ambapo jamii itaelimishwa ipasavyo juu ya sakata la uwekezaji kwenye bandari ya Daresalaam na serikali ya falme ya Dubai.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari, wabunge, wakuu wa wilaya na viongozi wa siasa mkoa wa Tanga, mini Korogwe.
Viongozi wa siasa wakisikiliza na kufuatilia mkutano.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji akiongea kwenye mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando akiongea kwenye mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments