Ticker

6/recent/ticker-posts

BARRICK BULYANHULU YAONGEZA NGUVU KAMPENI YA TOKOMEZA MALARIA MGODINI NA JAMII INAYOZUNGUKA MGODI

Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga wakishangilia kwa furaha baada ya kumaliza mbio za zenye urefu wa kilomita tano za kujenga afya ya mwili (Healthy Marathon) kuzunguka eneo la uzalishaji la mgodi huo, ikiwa ni uzinduzi wa kampeni maalumu ya kutokomeza ugonjwa wa malaria uliuofanyika mgodini hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga wakishiriki kukimbia mbio za kujenga ya mwili (Healthy Marathon) kuzunguka eneo la uzalishaji la mgodi huo, ikiwa ni uzinduzi wa kampeni maalumu ya kutokomeza ugonjwa wa malaria uliofanyika mgodini hapo.

Baadhi ya Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga wakipata mawaidha ya kulinda afya zao kutoka kwa mtaalamu wa afya kabla ya kuanza kukimbia mbio za uzinduzi wa kampeni maalumu ya kutokomeza ugonjwa wa malaria uliofanyika mgodini hapo.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo Victor Lule,alitoa zawadi kwa wafanyakazi walioshiriki kukimbia

Baadhi ya wafanyakazi katika picha ya pamoja baada ya kumalizika mashindano hayo

**

Wafanyakazi wa Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, uliopo halmashauri ya Msalala, wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga, mwishoni mwa wiki wameshiriki mbio za marathoni zenye urefu wa kilomita tano za kujenga afya ya mwili (Healthy Marathon) kuzunguka eneo la uzalishaji la mgodi huo, ikiwa ni uzinduzi wa kampeni maalumu ya kutokomeza ugonjwa wa malaria mgodini hapo.

Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo Victor Lule, amesema katika kukabiliana na ugonjwa wa Malaria mgodi huo umeanzisha kampeni maalumu ya Tokomeza Malaria kupitia marathoni ya mbio za kilomita tano ili kufikisha ujumbe kwa wafanyakazi wote na jamii inayozunguka mgodi huo.

Amesema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na menejimenti kuhakikisha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria yanadhibitiwa pia imehakikisha inahamasisha wafanyakazi wake kuvaa nguo za kuwakinga kung’atwa na mbu wanaoeneza Malaria nyakati za usiku.

Lule ambaye pia ni Meneja Operesheni wa mgodi huo amesema mbio hizo pia zimelenga kujenga afya za wafanyakazi na kupunguza uzito mkubwa unaopeleka magonjwa yasiyoambukiza.

“Leo tuliandaa mbio za kilomita tano kwa ajili ya wafanyakazi wetu wote ambao waliweza kujitokeza kushiriki mbio hizi lengo likiwa ni kushiriki kampeni yenye kauli mbiu Tokomeza malaria ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.” Alisema Lule.

Kwa upande Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Barrick Bulyanhulu, Dk. Kagodi Neg Kagodi, amesema katika kipindi cha mwaka huu maambukizo ya ugonjwa wa malaria yameongeza tofauti na mwaka jana ndio Mgodi huo umeamua kuja na kampeni maalumu ya kutokemeza ugonjwa huo.

Amesema uongozi wa Mgodi huo umechukua hatua mbalimbali za kupambana na ugonjwa wa malaria ikiwemo kupuliza dawa za kua mbu kwenye makazi ya watu katika vijiji vinavyozunguka mgodi na ndani ya mgodi, kugawa vyandarua kwa kila mfanyakazi pamoja na kuondoa madimbwi ya maji ambayo ndio mazalia ya mbu.

Amesema mazoezi ya kukimbia yaliyoshirikisha wafanyakazi yamelenga kuhamasisha wafanyakazi hao kuchukua tahadhali dhidi ya Malaria kwa kufuata maelekezo yote ya kujikinga ambayo yametolewa na wataalamu wa afya.

“Kampeni hiyo itasaidia kutokomeza kabisa maralia kama iliyo kauli mbiu yetu ya zero Malaria kwenye mgodi wetu inawezekana” alisema Dk. Kigodi

Baadhi ya wafanyakazi kutoka idara mbalimbali za mgodi huo ambao wameshiriki mbio hizo za marathoni wameishukuru kampuni ya Barrick Bulyanhulu, kuwaletea kampeni hiyo kwa kuwa imelenga kulinda afya zao.

Mmoja wa Wafanyakazi wa Mgodi huo, Emmanuel Mwakanyopole akiongea kwa niaba ya wenzake aliipongeza kampuni ya Barrick kwa kuwa na sera zinatotoa kipaumbele katika kujali afya na usalama wa wafanyakazi wake na wananchi wanaoishi kwenye jamii zinazozunguka migodi yake.

Post a Comment

0 Comments