Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Stergomena Tax kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Kituo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wameinadi Tanzania kama Kituo bora cha uwekezaji kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Italia.
Waziri Tax amewaeleza Wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kurekebisha sera na sheria mbalimbali ili kuwafanya wawekezaji wawe na mazingira bora ya kuendesha shughuli zao na hivyo kuvutia wawekezaji wengi zaidi.
Wafanyabiashara hao wameelezwa kuwa Tanzania ni salama kwa wao kuwekeza mitaji yao, ambapo pia watakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kulifikia na kunufaika na soko kubwa la EAC, SADC na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).
Miongoni mwa sekta zilizowavutia Wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Kilimo, Utalii, Viwanda, Uchumi wa Buluu, na Ujenzi.
Mkutano huo uliofanyika jijini Roma, Italia ulijumuisha Wafanyabiashara waliowekeza nchi Tanzania katika Sekta mbalimbali na wenye nia ya kuwekeza nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa omena Tax Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Mkutano na Wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza wakati wa Mkutano na Wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza wakati wa Mkutano na Wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji tanzania (TIC) Bw. Gilead Teri akizungumza wakati wa Mkutano na Wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Damas Mfugale akizungumza wakati wa Mkutano na Wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023
Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Khamis Dunia akizungumza wakati wa Mkutano na Wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na watendaji wa TIC, ZIPA na TTB waliposhiriki mkutano kati yao na Wafanyabiashara wa Italia uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023
0 Comments