Waziri wa Maliasili, Mhe. Mohammed Mchengerwa, jana Mei 6, 2023, amekutana na kufanya mazungumzo na mtoto mkubwa wa kiume wa Rais Mstaafu wa Marekani, Donald Trump, Donald Trump Junior, aliyeko nchini kufanya “Royal Tour.”
Katika mazungumzo hayo Waziri Mchengerwa alimweleza mgeni huyo mashuhuri mwelekeo wa sekta ya utalii na fursa mbalimbali za uwekezaji.
Kwa upande wake Bw. Trump Junior ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa nchini Marekani na ambaye pia anahudumu kama Makamu wa Rais Mwandamizi katika kampuni kubwa ya baba yake ya Trump Organization, akitajwa kuwa na utajuri unaogikia Dola Milioni 350 (zaidi ya Shilingi Bilioni 750), ameeleza kufurahishwa na Tanzania na kuahidi kutembelea maeneo mbalimbali zaidi ikiwemo Kadera/Kreta ya Ngorongoro.
0 Comments