Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI DKT. BITEKO AAGIZA UZALISHAJI KATIKA MGODI WA MWADUI UANZE


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  ( wa kwanza kushoto) akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi wa bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha akimuonesha eneo la bwawa jipya katika Mgodi wa Mwadui Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameagiza Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga kuanza shughuli za Uzalishaji kuanzia Julai 15 baada ya kuridhishwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa baada ya kingo za Bwawa la Maji Tope kubomoka.

Novemba 7,2022 Bwawa la tope la mgodini katika mgodi wa Mwadui lilipasuka na kuharibu makazi na mashamba ya wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze vilivyopo katika Kata ya Mwadui Luhumbo  wilayani Kishapu kwa kufunikwa na tope.


Akiwa katika Mgodi huo leo Ijumaa Juni 30, 2023 kwenye ziara yake ya kikazi, Waziri Dkt. Biteko ametoa agizo la uzalishaji kuanza baada ya kujionea hali halisi ya ujenzi wa bwawa la kuhifadhi tope laini la mgodini ambalo ujenzi wake umefikia 97% na bwawa la maji la wananchi la Ng’wang’holo ambalo ujenzi wake umefikia 98% pamoja asilimia 98% ya ulipaji fidia.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko

“Ulipaji wa fidia mbalimbali umefikia asilimia 96%. Kulikuwa na malalamiko 66 yameshashughulikiwa 61 bado matano ambapo tunaamini wiki inayokuja tutakuwa watakuwa wameyamaliza. Nimefurahi kuwa ujenzi wa bwawa la maji tope umekamilika tena limejengwa kwa Engineering tofauti na lililopasuka. Tutatoa vibali wiki inayokuja ili mgodi huu uanze mara moja”,amesema Waziri Biteko.

“Nachukua nafasi hii kumuomba Mhe. Mkuu wa Mkoa pengine tarehe 15 Julai 2023 kama ana nafasi aje ashuhudie kuanza kwa uzalishaji wa mgodi huu. Madini tunayoyategemea sana ni dhahabu aina ya pili tunayoyategemea kwa mapato ni almasi sasa kwa kipindi cha miezi sita tulisimama kwa sababu mara ya mwisho tumeenda sokoni ilikuwa Desemba hatujawahi kwenda tena kwa hiyo tumepotea sokoni kwa muda mrefu, tunatamani huu mgodi uanze mara moja ili turudishe mapato tuliyokuwa tunayapata lakini muhimu sana ajira za Watanzania ambao wapo kwenye mgodi huu zisipotee”,ameeleza Mhe. Biteko.

Ametoa kwa wito kwa mgodi huo uanze uzalishaji mara moja lakini waanze baada ya kuwa wamekamilisha taratibu zote za kuhakikisha kwamba linakuwa na bwawa imara.
Muonekano wa sehemu ya bwawa jipya katika Mgodi wa Mwadui

“Tunataka kuhakikisha kwamba tunakuwa na bwawa imara zaidi kuliko lililokuwepo na watuandikie kabisa commitment letter kwamba hili bwawa tunathibitisha na utalaamu halitaweza kuleta madhara, likileta madhara tujue tunawashughulikia kwa namna gani”,amesema Waziri Biteko.


“Namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alichukua muda kukutana na Mtendaji Mkuu wa Williamson Diamond Limited,alieleza matatizo yaliyopo katika Mgodi na Mhe. Rais akaahidi kwamba sisi tuyasimamie kwa haraka tuyamalize ili mgodi uanze kufanya kazi. Nataka nimhakikishie Mhe. Rais kwamba maelekezo yake tunayafanyia kazi na huu mgodi sasa unarudi kwenye Operation na sisi Wizara ya Madini ndiyo wasimamizi wa sekta hii tutahakikisha kila aina ya uchimbaji wa kufuata sheria na taratibu ili watu wabaki salama na fedha tuzipate, ajira zibaki, kodi tupate vyote vinazingatiwa”,ameongeza.


Amewashukuru wananchi kwa utulivu wao pamoja na Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, serikali ya Mkoa , Wilaya kwa usimamizi wa karibu wa jambo hilo vinginevyo lingezua matatizo mengi na mijadala mingi.


Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda amesema wapo tayari kuanza uzalishaji muda wowote wanachosubiri ni kibali tu.
“Ujenzi wa bwawa la maji ya wananchi Ng’wang’holo umefikia asilimia 98, bwawa la kuhifadhi tope laini la mgodini asilimia 97 na 96% ya utoaji fidia mbalimbali kwa wananchi ambazo ni mali, vitega uchumi, chakula na kodi kwa walioathirika kwenye makazi. Makazi 47 yatajengwa kuanzia mwezi Julai 2023 kipindi cha miezi 6”,amesema Mhandisi Mwenda.


“Baada ya kutokea kwa tukio hili taharuki ilitoke lakini serikali imekuwa karibu nasi kulishughulikia, na tunashukuru pia wananchi wamekuwa watulivu. Tangu bwawa lipasuke hatukuwahi kufanya uzalishaji, kwa kweli hili ni pigo kwetu na wafanyakazi wetu. Tunashukuru sana shughuli za uzalishaji kurejea na tunaahidi hadi kufikia Julai 15 tutakuwa tumeanza kufanya kazi”,amesema Mhandisi Mwenda.


Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Modest Mkude wamesema kuanza kwa uzalishaji katika mgodi huo kutasaidia kurudisha ajira na mapato yaliyokuwa yamepotea huku wakiomba wananchi waendeleee kutoa ushirikiano ili amani na mshikamano uendelee kuwepo.


Katibu wa Chama cha Wachimbaji wa Wadogo wa Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kigosi wameuomba mgodi wa Almasi Mwadui uwapatie kituo cha maji (DP) katika mgodi wa Ng’wang’holo ambapo mgodi huo umekubali ombi hilo.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha akimuonesha eneo la bwawa jipya katika Mgodi wa Mwadui Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Muonekano wa sehemu bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi wa bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  (katikati) akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi wa bwawa jipya la tope laini la mgodini katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 


Mbunge wa Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Modest Mkude akizungumza wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Katibu wa Chama cha Wachimbaji wa Wadogo wa Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kigosi  akizungumza wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza wakati Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akitembelea Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) 
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akiangalia bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Ijumaa Juni 30,2023.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  akimwelezea Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuhusu ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akizungumza katika eneo la ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akiondoka katika eneo la ujenzi sehemu ya kuchotea maji katika bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Sehemu ya bwawa la wananchi Ng'wang'holo katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited)
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda  akimuonesha Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kitalu cha kuoteshea miti katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited).

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



Post a Comment

0 Comments