Waziri wa Maji Jumaa Aweso(Mb) amemuahidi Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe.Salim Alaudin Hasham kuwa atatoa ushirikiano wa kina yeye na ofisi yake katika mapambano ya kuhakikisha wilaya ya Ulanga inamaliza Changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Waziri Aweso ameyasema hayo wakati alipotembelewa Ofisini kwake Dodoma na Mbunge Salim akiwa na wafadhili kutoka Uswisi ambao wamekuja kwa lengo la kuangalia Changamoto ya maji wilayani Ulanga ili kuona namna bora ya kuisaidia kuondokana na shida hiyo.
Naye mfadhili wa maswala ya maji kutoka nchini Uswisi Bi. Rubab Jawad Aziz amesema kilichomvutia kusaidia wilaya ya Ulanga kuondokana na tatizo la maji ni kwasababu wazazi wake waliishi hapo na yeye alilelewa hapo hivyo anajua Changamoto hizo tangu akiwa mtoto mdogo kabla ya kwenda nje ya nchi kutafuta maisha.
Kwa upande wake Mbunge Salim amesema lengo la kutafuta wafadhili kwa wingi ni kuona namna bora ya kuisaidia Serikali katika kutatua Changamoto mbalimbali.
Jimbo la Ulanga linazalisha kiasi cha lita 8000 hadi 9000 wakati mahitaji ya maji ikiwa ni lita 1,600,000.
0 Comments