Na Chalila Kibuda
Watumishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wameaswa kuzingatia mazoezi ya mara Kwa mara ili kuboresha afya za miili yao na akili vitakavyowawezesha kufanya kazi Kwa bidii, weledi na kuongeza tija mahala pa kazi
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Uchukuzi Ndugu Lucas kambelenje ambaye pia ni mlezi wa Timu za Uchukuzi Sports Club wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Saba la Michezo linakohusisha timu za Wizara Sekta Uchukuzi na Taasisi zake ambalo limeandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)wa lililofanyika kwenye Viwanja vya TCC Gwambina, Chang'ombe Jijini Dar es salaam
"Michezo ni afya na nisehemu ya kutengeneza mahusiano ya kikazi hivyo nasisitiza Viongozi wanaosimamia timu za UChukuzi kuhakikisha mashindano kama haya yanayohusisha Wizara na Taasisi zake yanafanyika mara Kwa mara ili kujenga afya za mwili na akili Kwa Watumishi na hii itasaidia kuwaongeza Ari na Motisha katika utendaji kazi wao wa Kila siku" amesisitiza Kambelenje
Akijibu kuhusu changamoto zinazozikabili timu za UChukuzi Sports Club. Zinapokuwa kwenye uwakilishi wa mashindano mbalimbali Nchini Kambelenje amesema Wizara itaendelea kuwasisitiza h Wakurugenzi wa Taasisi zote zilizo chini ya Sekta ya Uchukuzi ili wazidi kusapoti na kuwezesha Kwa wakati Watumishi kushiriki Mashindano mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika Nchini ili timu za UChukuzi ziendelee kuwa kinara kama ilivyo sasa
Akizungumzia ufinyu wa bajeti na Watumishi kukosa ruhusa jambo linalosababisha timu kushindwa kushindana hususan kipindi hiki ambapo Kuna timu za Majeshi zinazojiandaa vyema amesema suala hilo amelipokea na ataliwasilisha Kwa mamlaka za juu za Wizara ili liweze kufanyiwa kazi Kwa haraka kwani lengo la Wizara ni kuhakikisha timu za UChukuzi Sports Club zinaendelea kuwa washindi wa kwanza kama ilivyokuwa awali Kwa miaka ya 2020,2021 na 2022
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi , Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Kwa njian ya maji(TASAC) Ndugu Nelson Mlari ameushukuru Uongozi mzima wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Kwa kuendelea kutekeleza agizo la Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan la kudumisha Michezo mahala pa kazi kwani Kuna tija kubwa na inasaidia sana watumishi kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo ni tishio Kwa sasa
Akitoa salamu Kwa niaba ya Wakurugenzi wa Sekta za UChukuzi, Mkurugenzi wa kiwanja Cha Ndege Cha Kimataifa Cha Arusha(CADCO) Ms.Christine Mwakatobe amesema kama viongozi wa Taasisi za UChukuzi wamepokea changamoto zote ambazo ziko Ndani ya uwezo wao kama kutenga bajeti toshelevu na ruksa Kwa wakati Kwa Watumishi na ataziwasilisha hoja hizo haraka kwenye vikao vya Wakurugenzi vya utawala ili vifanyiwe kazi mapema Kwa ajili ya mashindano yajayo ya Shimiwi yanayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba, 2023 ili timu za Sekta za UChukuzi ziweze kuwa na ushindani wa kweli utakaoleta vikombe zaidi ya mashindano ya Mei Mosi yaliyopita
Naye Katibu wa Timu za Uchukuzi Sports Club, Ndugu Mbura Tenga amesema, kwenye mashindano ya Mei Mosi yaliyofanyika Mkoani Morogoro mwezi April, 2023 timu za Sekta ya Uchukuzi zilifanikiwa kushinda vikombe 8 kati ya vikombe vyote vya jumla 14 vilivyokuwa vikishindaniwa ambapo vitatu ni vya Mshindi wa kwanza Kwa upande wa kamba Wanawake na Wanaume na Tufe Wanaume na kuibuka Mshindi wa pili katika washindi wa jumla huku akitaja changamoto za ufinyu wa bajeti , ucheleweshaji wa michango kutoka Taasisi za UChukuzi na ruhusa Kwa Watumishi vikichangia kupunguza morali Kwa wachezaji.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Uchukuzi Ndugu Lucas kambelenje akizungumza wakati Tamasha la Michezo la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Uchukuzi lililoratibiwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na kufanyika Viwanja vya TCC Gwambina jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Uchukuzi Ndugu Lucas kambelenje akimvisha medali wana michezo upande wa wanawake wakati Tamasha la Michezo la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Uchukuzi lililoratibiwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na kufanyika Viwanja vya TCC Gwambina jijini Dar es Salaam.
Baadhi picha za mazoezi katika tamasha la michezo Sekta ya Uchukuzi lililoratibiwa na TASAC , jijini Dar es Salaam
Baadhi watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Uchukuzi wakiwa katika tamasha la Michezo lililoratibiwa na TASAC
0 Comments