Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI ZAIDI YA ELFU 16 KARAGWE KUONDOKANA NA ADHA YA MAJI.


Na Shemsa Mussa, Kagera .

Zaidi ya Shiling Bilion 6.7 zitatumika katika utekelezaji na ujenzi wa miradi mitatu 3 mikubwa ya maji katika wilaya ya Karagwe Mkoani kagera .
Akibainisha hayo Meneja wa RUWASA Wilaya ya karagwe Mhandisi Cassian Witike katika hafla ya utiaji saini wa Makubaliano ya ujenzi wa miradi hiyo kati ya serikali na RUWASA na kusema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetengwa kwa ajili ya miradi ya maji ndani ya wilaya hiyo.

Bw,Witike ameitaja miradi hiyo kuwa ni Omukime, Rwamugulusi na Chanika - Runyaga ambayo inatarajiwa kuwahudumia wananchi zaidi elfu 16 na amewasihi wananchi kukubali kupisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi huo wa maji ambayo itawanufaisha wenyewe na ujenzi huo utakamilika ndani ya miezi 6

"Tunaomba wananchi waipokee hii miradi na tumeshasema miradi hii haina fidia kwenye maeneo yale yote ambayo tunaenda kujenga miundombinu ya maji, tutajenga matenki , tutajenga vituo vya kuchotea maji na tutalaza mabomba yenye urefu zaidi ya kilometa hamsini 50 kwenye miradi yote, amesema Witike" .

Nae Mkuu wa wilaya ya Karagwe Mhe Julius Laizer ameitaka Mamlaka hiyo kuwashirikisha wananchi kwa kila hatua ya ujenzi huo wa miradi ya maji ili kuifanya iwe salama na endelevu pindi itakapokamilika .

"Lazma mikutano ya hadhala ya kijiji husika iwepo kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi wananchi waambiwe Fedha imetoka wapi na ni kiasi gani mkandarasi ni yupi ili nao wajue nini kinaendelea. amesema Laizer".

Nao baadhi ya Madiwani wa wilaya hiyo wamewataka wananchi kuitunza na kuilinda miradi hiyo pindi itakapokamilika ili kudumu kwa muda mrefu na kupunguza adha ya maji katika baadhi ya maeneo .

Post a Comment

0 Comments