Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKUU WA MIKOA WAOMBWA KUTOA ELIMU KUHUSU ULINZI,USALAMA NA USTAWI WA WAZEE


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, jijini Dodoma leo Juni 7,2023 kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma Mzee Peter Mpolo,akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, jijini Dodoma leo Juni 7,2023 kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.


Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati ,akizungumza nao jijini Dodoma leo Juni 7,2023 kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja na wazee mara baada ya kuzungumza a na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, jijini Dodoma leo Juni 7,2023 kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha elimu ya kina inatolewa kwa wananchi juu ya haki, ulinzi, usalama na ustawi wa wazee.

Waziri Gwajima ameyasema hayo leo Juni 7,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, Mkoani Dodoma kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.

Dkt. Gwajima amesema kuwa kutokana na kuboreshwa kwa huduma mbalimbali za kijamii nchini idadi ya wazee imeongezeka kutoka 2,507,568 hadi kufikia 5,008,339 ambayo ni sawa na asilimia 8.1 ya Watanzania 61,741,120.

Amesema Serikali imeendelea kuadhimisha Siku ya kupinga Ukatili Dhidi ya Wazee kila tarehe 15, Juni ambapo Maadhimisho haya muhimu kwa ajili ya kuuhabarisha umma juu ya haki, ulinzi, maendeleo na ustawi wa wazee wetu. Aidha, katika kulinda haki ya wazee kuishi, pia Serikali imeendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji kwa Wazee

"Ninachukua fursa hii pia kuwaomba Wakuu wa Mikoa yote nchini kuratibu maadhimisho haya kimikoa kwa kushirikiana na viongozi wa Mabaraza ya Wazee katika mikoa husika. Katika maadhimisho haya" amesema Waziri Dkt. Gwajima.

Waziri Gwajima ameendelea kusisitiza jamii yote kuacha kufanya ukatili kwa Wazee na makundi yote kwa ujumla na amewaomba Wanahabari kutumia vyombo vyao kuelimisha na kuendelea kukemea masuala ya ukatili nchini kote.

"Serikali itaendelea kuchukua hatua stahiki kuwashughulikia ipasavyo wale wote watakaobainika kufanya vitendo vya ukatili kwa makundi mbalimbali katika jamii hususani kwa wazee". ameongeza Waziri Dkt. Gwajima.

Maadhimisho ya Kupinga ukatili Dhidi ya Wazee mwaka huu yatafanyika katika ngazi ya Mikoa kote nchini na Kaulimbiu ni "Wazee Wanastahili Heshima na Usikivu Wetu”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma Peter Mpolo ameipongeza serikali kwa kuendelea kuwajali wazee kwa kuwapatia huduma mbalimbali ambazo zinawafanya waendelee na shughuli mbalimbali.

" Kila mzee anapaswa kurudi kwenye jukumu la kutunza watoto kwa kuwafundisha mila na desturi za kitanzania."amesema Mzee Mpolo

Post a Comment

0 Comments