SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limepokea mabehewa sita ya ghorofa kati ya 30 yameboreshwa na kampuni ya Luckmier Transport & Logistic ya Ujerumani leo Juni 9,2023.
Akizungumza wakati wa kupokea Mabehewa hayo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete amesema kuwa Mabehewa hayo yametengenezwa kisasa ambayo hata ukienda kwenye nchi za wenzetu ni mazuri zaidi maana yamefanyiwa ukarabati zaidi ya asilimia 80.
Mabehewa hayo yapo katika madaraja mawili yaani daraja la pili ambalo linachukua watu 123 na daraja la tatu linauwezo wa kuchukua watu zaidi ya 140 utofauti uliopo kati ya daraja moja na jingine ni ukubwa wa nafasi kubwa zaidi na katika daraja la tatu nafasi yake nikubwa kidogo lakiniubora wake kama upo ndani ya basi ama upo ndani ya ndege kwawale mmetumia usafiri wa ndege.
Amesema kuwa wizara kupitia na TRC la tumekusudia kufanya majaribio mwezi wa saba mara tuu kichwa kitakapowasilia nchini.
Mwakibete ametoa rai kwa watanzania juu ya utunzaji wa mabehewa hayo pale tuu yatakapoanza kutumika.
"Tuzitunze rasilimali za nchi sio kwenda kuandika na kuyachubua ndani sababu gharama ya ukarabati imefanyika ni kubwa na ni kodi za watanzania."
Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewapa dhamana Wizara ya ujenzi na uchukuzi kusimia shirika la TRC.
"Tunategemea pia kupata vichwa vingine vya kutoka Kampuni ya Hyundai kutoka Korea Kusini ambayo ilishinda zabuni kwa ajili ya kutengeneza jozi 10 za treni za EMU (Electric Multiple Unit), kwa ajili ya shughuli za uendeshaji katika reli ya kisasa - SGR ambayo treni zake zitatumia umeme.
"Tunategemea kupata mabehewa mengine ya kisasa kwahiyo nimeridhishwa na nimefurahi kwa mara ya kwanza kwenye nchi yetu tangu reli ya kikoloni, reli ya uhuru tulijenga wenyewe lakini reli hi ya awamu ya sita tunapata mabehewa ya ghorofa." Amesema
Kwa Upande wa Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa ni mabehewa sita ya ghorofa kati ya mabehewa 30 na vichwa viwili ambavyo kampuni ya Eurowagon ya nchini Uturuki ilishindwa kukamilisha ujenzi wa vichwa vya treni ya umeme na serikali ikavunja mkataba huo na kusaini mkataba na Kampuni ya Ujerumani ambapo yamenunuliwa hayo.
Amesema Mabehewa hayo yataendelea kuletwa nchini pale yanapokamilika ili kuweza kufanya majaribio katika reli ya Kisasa ya SGR licha ya kupata changamoto ya UVIKO-19.
"Serikali iliamua kuleta mabehewa yaliyotumika baada ya kuwa yamefanyiwa ukarabati mkubwa, na sisi watanzania sio wa kwanza kutumia mabehewa yaliyokarabatiwa, China, Marekani nao wananunua mabehewa yaliyotumika na yanakarabatiwa." Amesema Msigwa
Amesema mabehewa hayo yatasubiri kichwa cha treni kitakachowasili mwanzoni mwa Julai ambapo majaribio yataanza kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro
Amesema hadi kufikia Novemba mwaka huu Mabehewa yote yatakuwa yamewasili nchini pamoja na Vichwa viwili na kazi ya kubeba abiria kwenye kipande cha kwanza cha Dar Es Salaaam kwenda Morogoro na Kipande cha Morogoro Makutupora.
"Abiria watakuwa na uwezo wa kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia reli yetu na mabehewa ndio haya yameshawasili na kumekabidhiwa." Amesema Msigwa
Akizungumzia kuhusiana na Utunzaji wa Mabehewa, mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Masanja Kadogosa amesema kuwa watayatunza kwaajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Amesema ujio wa Mabehewa hayo unaweza kuwa mazuri wa Watanzania kuliko mapya ambayo yatakuja na behewa moja kati ya mabehewa hayo sita ni sawa na Mabasi matatu kwa uwezo wa kubeba abiria.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete akikata utepe kuashiria Upokeaji wa Mabehewa sita ya ghorofa kati ya 30 yameboreshwa na kampuni ya Luckmier Transport & Logistic ya Ujerumani mabehewa hayo yamepokelewa leo Juni 9,2023.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi, Atupele Mwakibete akizungumza wakati wa Upokeaji wa Mabehewa sita ya ghorofa kati ya 30 yameboreshwa na kampuni ya Luckmier Transport & Logistic ya Ujerumani mabehewa hayo yamepokelewa leo Juni 9,2023.
Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza wakati wa Upokeaji wa Mabehewa sita ya ghorofa kati ya 30 yameboreshwa na kampuni ya Luckmier Transport & Logistic ya Ujerumani mabehewa hayo yamepokelewa leo Juni 9,2023.
Ukarabati uliofanywa ndani ya Mabehewa sita kati ya 30 kutoka nchini Ujerumani.
Baadhi ya Mabewa yaliyokarabatiwa kutoka nchini Ujerumani.
0 Comments