Na. Peter Haule, WFM Dodoma.
Tanzania imepokea msaada wa paundi milioni tano sawa na takribani shilingi bilioni 15 kutoka Serikali ya Ungereza kwa ajili ya awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF).
Makabidhiano ya Hati za makubaliano ya msaada huo yamefanyika jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Dkt. Mwamba alisema kuwa utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini Tanzania unaendelea vizuri jambo linalosababisha washirika wa maendeleo kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya mpango huo.
Alisema kuwa amekutana na Balozi huyo wakiangazia masuala ya kunusuru kaya maskini lakini pia kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizo mbili ambao umedumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, alisema Uingereza ni rafiki mkubwa wa Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo, hivyo nchi yake itaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha inatoa mchango wake katika kukabiliana na umasikini ili kuboresha hali ya maisha ya wananchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, wakipeana mikono baada ya kubadilishana Hati za makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, wakionesha Hati ya makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati za msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), iliyofanyika jijini Dodoma.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akizungumza kuhusu nchi yake kuendelea kuisaidia Tanzania katika kupunguza umasikini, wakati wa hafla ya kubadilishana hati ya makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya TASAF, iliyofanyika jijini Dodoma.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba (kushoto) na Ujumbe wa Uingereza Ukiongozwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati ya makubaliano ya msaada wa takribani shilingi bilioni 15 kwa ajili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), hafla iliyofanyika jijini Dodoma
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)
0 Comments