Ticker

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA TAALUMA YA MAENDELEO YAADHIMISHA MIAKA 50

TAASISI ya Taaluma za Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IDS) imeadhimisha miaka 50 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1973 kwa kuyafikia mafanikio makubwa ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha inaendelea kuwa mfumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayowakabili watanzania na waafrika ili kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo juni 30, 2023 jijini Makamu mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam (UDSM) Prof .William Anangisye amesema kuwa lengo la taasisi hiyo katika siku zijazo nikuwaleta Pamoja wanataaluma na IDS imeendelea kutoa mchango mkubwa kwa taifa, pia kutoa fursa kwa wanataaluma kufanya tafakuri nini kimefanyika, tuko wapi na nini kifanyike kwa miaka 50 ijayo kwaajili ya manufaa ya watanzania

“Tunataka tufanye hii taasisi iwe kituo cha kuwaleta Pamoja wanataaluma, wasomi kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu ili kusaidiana na kukumbushana kwa pamoja namna mzuri ya kuweza kuchangia katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayowakabili wa afrika” amesema Prof William Anangisye

Aidha, Prof . Anangisye amesema katika suala zima la kutoa huduma kwa watanzania wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tunatafuta ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili pia watu wajue lazima tufanye kazi kwa sababu maendeleo hayaji kwa kukaa ndani au chini ya mti kuyasubiria yaje.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo (UDSM) Dkt. Colman Msoka amesema kuwa kwa muda wa miaka 50 taasisi hiyo imefundisha watu wengi na kupata mafanikio makubwa ikiwemo mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya na wakuu wa wa mikoa lengo la taasisi hii ilikuwa nikuwajengea wanafunzi wa chuo kikuu uwezo wa kutumia taaluma zao mbalimbali walizosomea katika vyuo.

Ameongezea kuwa Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo (IDS) ni kisima cha fikra cha maendeleo na imeendelea pia kutoa mchango kwa serikali “tunafanikio makubwa, taasisi imeendelea kuwepo somo hili kwa wanafunzi wote wanaopita Dar es salaam wamekuwa wanasoma na wametuletea mrejesho jinsi kozi za maendeleo zimekuwa zikiwapa manufaa na uwezo kwa kutenda kazi zao” amesema Msoka

Hivyo, baadhi ya wanafunzi wa taasisi hiyo wamesema kuwa kozi imekuwa msaada mkubwa kwa kupata uelewa juu ya dunia inapoelekea na imekuwa faida kwao kwa kuwafanya wanafunzi kutokuwaza ajira na kuweza kujiari wenyewe pia wametumia nafasi kuishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele kozi hiyo tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Post a Comment

0 Comments