Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YASAINI MAKUBALIANO NA UNESCO KUINUA SEKTA YA HABARI

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini Makubaliano ya Ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni-UNESCO yatakayosaidia kuimarisha uchumi na Uhuru wa vyombo vya Habari.

Akizungumza leo Juni 3,2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa makubaliano hayo yatachochea kuimarisha usalama wa wandishi wa habari wanapotimiza majukumu yao.

“Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo kupitia UNESCO, tunalenga pia makubaliano haya yatasaidia kutoa mafunzo na kuwaendeleza Waandishi wa Habari, kutakuwa na mafunzo mablimbali ambayo yatadhaminiwa na UNESCO kwa lengo la kuboresha sekta hii,” Amesema Waziri Nape.

Aidha amesema makubaliano hayo yanalenga kuimarisha mazingira ya kisera na kisheria na tayari Serikali ya Tanzania ilishachukua hatua kadhaa ambapo hivi sasa mchakato wa kupitia sera sheria na kanuni unaendelea ambapo mchakato wa sheria tayari upo bungeni kwenye hatua za mwisho.

Amesema , jambo lingine ni kuangalia usalama na ulinzi wa waandishi wa habari hasa wanapokuwa kwenye kutimiza majukumu yao sambamba na kuimarisha taaluma ya habari kwa kuimarisha mifumo ya kudijitali na kusisitiza kwamba makubaliano hayo yatatoa msukumo kwa Sekta nzima ya habari nchini ili isiachwe nyuma.

Kwa upande wake Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, Bw.Michael Toto amesema mkakati huo unatoa mwongozo wa ushirikiano kati ya UNESCO na Serikali ya Tanzania pamoja na taasisi nyingine za Umoja wa Mataifa na wadau wa maendeleo na kwamba hiyo ni hatua muhimu kuelekea utatuzi wa changamoto zinazoikabili sekta ya habari.

“Nina furaha kuthibitisha utayari wa UNESCO kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiano na Teknolojia ya Habari katika kushughulikia maeneo yote ya kipaumbele katika makubaliano haya, tutafanikiwa ikiwa Watanzania wote watashirikishwa kwenye hatua za maendeleo kwa uhuru ambapo hakuna atakaeachwa nyuma kwa kuwa wote watakuwa na taarifa sahihi, bora na watazipata kwa wakati,” alisema Toto.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye(kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, Bw.Michael Toto wakisaini Makubaliano ya Ushirikiano yatakayosaidia kuimarisha uchumi na Uhuru wa vyombo vya Habari. Hafla iliyofanyika leo Juni 3, 2023 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye(kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, Bw.Michael Toto wakipongezana mara baada ya kusaini Makubaliano ya Ushirikiano yatakayosaidia kuimarisha uchumi na Uhuru wa vyombo vya Habari. Hafla iliyofanyika leo Juni 3, 2023 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, Bw.Michael Toto wakionesha mkataba waliosaini utakaosaidia kuimarisha uchumi na Uhuru wa vyombo vya Habari. Hafla iliyofanyika leo Juni 3, 2023 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO yatakayosaidia kuimarisha uchumi na Uhuru wa vyombo vya Habari. Hafla iliyofanyika leo Juni 3, 2023 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, Bw.Michael Toto akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yatakayosaidia kuimarisha uchumi na Uhuru wa vyombo vya Habari. Hafla iliyofanyika leo Juni 3, 2023 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mohammed Abdulla akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO yatakayosaidia kuimarisha uchumi na Uhuru wa vyombo vya Habari. Hafla iliyofanyika leo Juni 3, 2023 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, Bw.Michael Toto, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Mohammed Abdulla na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali GERSON MSIGWA. Mhe.Gerson Msigwa wakipata picha ya pamoja na watumishi kutoka UNESCO pamoja na watumishi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika hafla ya utiaji saini Makubaliano ya Ushirikiano yatakayosaidia kuimarisha uchumi na Uhuru wa vyombo vya Habari. Hafla iliyofanyika leo Juni 3, 2023 katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments