Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA KITAIFA YA KUPIGA VITA MATUMIZI NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA DUNIANI, MKOANI ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya Wataalamu waliopo kwenye Banda la Maonesho la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kuhusiana na kazi mbalimbali ambazo Mamlaka hiyo inafanya katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha tarehe 25 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko kuhusiana na kazi ambazo Ofisi yake inafanya ikiwemo uchunguzi wa kimaabara wa vielelezo mbalimbali ikiwemo dawa za Kulevya katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha tarehe 25 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya Wataalamu mbalimbali waliopo kwenye Mabanda ya Maonesho katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha tarehe 25 Juni, 2023.
Vikundi mbalimbali vya Vijana vikipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan huku wakionesha ujumbe mbalimbali katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha tarehe 25 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya Maadhimisho ya Kitaifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Jijini Arusha tarehe 25 Juni, 2023.
Viongozi mbalimbali wa Dini, Serikali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Arusha wakiwa ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid kushiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani humo 25 Juni, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Banda la Maonesho la Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Mkoani Arusha 25 Juni, 2023.

Wasanii Mbalimbali Joh Makini, Diamond pamoja na Mrisho Mpoto wakitumbuiza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha tarehe 25 Juni, 2023.

Post a Comment

0 Comments