Na Magrethy Katengu
Msemaji Mkuu wa serikali Gryson Msigwa amesema amekanusha upotoshaji Mkubwa unaondelea katika mitandao ya kijamii kuwa bandari imeuzwa kwa kampuni ya DP World kutoka Serikali Dubai kwa miaka 100 jambo hilo halina ukweli ndani yake atoa ufafanuzi wa kina.
Akizungumza na Waandishi wa habari wa kimtandao (JUMIKITA) Jijini Dar es salam amesema mazungumzo yanayoendelea Sakata la makubaliano ya ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai katika uendeshaji wa bandari nchini na limeendelea kuibua mijadala nchini, hasa mitandaoni
Mijadala hiyo inaibuka wakati Bunge kupitia kwa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) likipokea maoni ya kuridhia makubaliano hayo yanayoelezwa na Serikali kuwa yatachochea ufanisi wa huduma mara utekelezaji utakapoanza.
"Taarifa sahihi ni Makataba ambao unazungumzwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia makubaliano na Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi 12kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Serikali ya Tanzania kujadiliana na Serikali ya Dubai kuhusu maeneo ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika uboreshaji wa Sekta ya Bandari nchini Tanzania"amesema Msigwa
Sambamba na hayo amefafanua kwenye mkataba huo ndiyo kunatoa nafasi kuingia mikataba mingine na kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 63 kifungu cha( 3)(3) inaelezwa kunapokuwa na mkataba wa makubaliano kati ya nchi na nchi mkataba unatakiwa kupelekea bungeni ili wabunge wakajadili na kutolewa maoni na kuruhusu serikali iweze kuendelea na mikataba ya utekelezaji na tumepewa miezi 12 ya mazungumzo kama hatujakamilisha mkataba huo unakuwa umekufa .
Hata hivyo amebainisha kuwa Bandari ya Dar es salaam imekuwa na changamoto kubwa ya ufanisi mdogo na juhudi kubwa zimefanyika ikiwemo kuongeza kina cha maji na mpaka sasa bandari hiyo Ina uwezo wa kuhudumi chini ya tani milioni 20 kwa mwaka kiwango hiko kikilinganishwa na fursa zilizopo ni kidogo mno tafiti zilifanyika na Wataalamu walituambia tukiwekeza kwenye bandari ipasavyo inaweza kuhudumia tani milioni 58 kwa mwaka na ili ifikie huko inahitajika uwekezaji.
Sanjari na hayo Msigwa amesema Wataalamu waliwaeleza pia iliwafikie kiwango cha kuhudumia tani milioni 58 kwa mwaka inahitajika uwekezaji si chini ya trillion moja na kazi inayoendelea ya kuongeza kina cha bahari serikali imekopa fedha si chini ya trillion 1 na gati mpya Moja limeshajengwa la kushusha magari lakini pia kina cha bahari kimeshaongezwa kuanzia gati namba 1mpaka namba 7 na tunaendelea gati hadi la 11 yaani hilo eneo dogo moja imetumika zaidi ya trillion 1 hivyo inahitajifa uwekezaji.
"Kama tukichukua fedha za wananchi za kuwapatia huduma ikiwemo kupeleka huduma kwa wananchi umeme, maji, barabara, shule , zahanati hivyo serikali iliona mbali ikasema kwa nini wasitumie sekta binafsi isaidie kuwekeza kwenye sekta ya bandari na itasaidia kupata fedha na serikali isaidie jamii kuipa huduma" amesema Msemaji Mkuu wa serikali.
Pia amebainisha kuwa mwaka 2021/2022 bandari ya Dar es salaam uzalishaji ulikuwa trillion 1.08 mwaka mzima na matumizi zaidi ya bilioni 900 na fedha kubwa inakwenda kwenye uendeshaji na fedha inayobaki haizidi bilioni 120 sasa umuhimu wa bandari yote hii inabakia kupata bilioni 120 hivyo tutambue bandari haina ufanisi.
Msemaji Mkuu wa serikali amesema Serikali inatafuta kwanza mwekezaji mwenye tija na mtaji mkubwa na wataalamu waliwaambia wakiwa na muwekezaji wanaweza kukisanya mapato zaidi ya mara miambili ya haya yanayopatikana sasa na ndiyo serikali ikaona bora ifanyike uwekezaji na ndiyo Duniani wanavyofanya nchi zilizo na bandari
Aidha amesema wamezungungumza na Makampuni mengi ikiwemo China, Ujermani na wakaona Kampuni ya DP World kutoka Falme za Kiarabu kwani mizingo mingi inatokea Dubai na hawa ndipo walipo na hawa bado hatujafunga nao mkataba ila kwa kweli tumeona ni watu ambao tukifanya nao kazi tutapata manufaa makubwa
Aidha niwatoe hofu wananchi kuwa Serikali ipo macho na Wataalamu Wapo hakuna mkataba mpaka sasa uliosainiwa na itakapofika hapo kwenye kusainiana mkataba na kuendesha bandari zetu ili upatikanike ufanisi zaidi tutafanya mikataba yenye kulinda maslahi ya watanzania na mikataba itafanyika kwa uwazi hiki kinachoendelea ni mashirikiano tupo kwenye mazungumzo Bunge lipo kwenye mchakato.
0 Comments