Ticker

6/recent/ticker-posts

MILANGO KWA UWEKEZAJI BIASHARA YA KABONI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amesema Serikali inaendelea kufungua milango kwa wawekezaji wa Biashara ili kuhifadhi mazingira.

Amesema hayo leo Juni 06, 2023 wakati wa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora Dkt. Rashid Chuachua pamoja na ujumbe wake waliomtembelea kwa Kuwasilisha taarifa ya kusudio la kuanzisha mradi wa hifadhi ya misitu kwa ajili ya biashara ya kaboni.

Ameupongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa kuhifadhi misitu na nia yao ya kuwekeza katika biashara ya Kaboni akisema kuwa mbali ya kuhifadhi mazingira lakini pia itawa chanzo cha mapato ya halmashauri.

“Kutokana na Mikataba ya Kimataifa ya Mabadilkiko ya Tabianchi, sisi kama nchi tumejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanafaidika na biashara hii na ndio maana tumeandaa kanuni na mwongozo,” amesema.

Pia, amesema Ofisi ya Makamu wa Rais ipo tayari kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kuwapa uelewa wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini zikiwemo halmashauri kuhusu faida za kupanda miti na kuhifadhi misitu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Chuachua amesema kusudio la kuanzisha mradi wa hifadhi ya misitu kwsa ajili ya hewa ya ukaa ni kupata fursa ya biashara hiyo ambayo faida yake itasaidia kuboresha huduma kwa wananchi wake.

Amesema wilaya ina fursa kubwa ya kuwekeza katika biashara hiyo kwa kuzingato kuwa kilomita za mraba 12,084.5 sawa na asilimia 86 ya eneo lote la wilaya hiyo.

Hivyo amesema kuwa mradi huo ni muhimu kwan utasaidia kuongeza wigo wa mapato ya halmashauri ambayo kwa asilimi 80 yaekuwa yakitona na mazao ya kilimo.

Dkt. Chuachua ameongeza kwa kusema kuwa mradi utasaidia katika kutunza mazingira ya ardhi oevu ambayo ndio chanzo cha maji katika Mto Malagarasi na Ziwa Tanganyika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba amesema kuwa Biashara ya Kimataifa inasimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo kuwezesha nchi wanachama kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Komba amesema kuwa mabadiliko ya tabianchi yanasababisha ongezeko la joto duniani na vipndi vya baridi na mvua kupungua hali inayochangia ukame.

Hivyo amesema misitu ikiwa mingi itasaidia katika kunyonya gesijoto inayochangiwa na shughuli za kibinadamu zikiwemo moshi unaotokana na magari na viwanda.



Post a Comment

0 Comments