Unaweza kusema hayawi hayawi yamekuwa hii ni baada ya mabehewa sita ya ghorofa kati ya mabehewa 30 kwa ajili ya reli ya kiwango cha SGR tayari yamewasili kwenye Bandari ya Dar es salaam yakitokea nchini Ujerumani leo June 6 2023 Mabehewa hayo yakiwa aina mbili ambapo daraja la pili lina uwezo wa kubeba abiria 123 na daraja la tatu lina uwezo wa kubeba Watu 140.
Pia Mabehewa hayo yameboreshwa na kampuni ya Luckmier Transport & Logistic ya Ujerumani ambapo mabehewa 24 yaliyosalia na vichwa viwili bado matengenezo yake yanaendelea.
Kuwasili kwa mabehewa haya ni ishara ya kujiandaa na kuanza kwa safari za treni ya kisasa ambapo itakumbukwa hivi karibuni Serikali ilisema reli ya kisasa ya SGR kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro (KM 300) itaanza majaribio mwezi wa saba na kutoa huduma mara baada ya majaribio kukamiilika mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete akijibu swali Bungeni aliahidi kwamba mwezi wa sita wanategemea kupokea mabehewa yenye ghorofa na mwezi wa saba mwishoni watapokea kichwa ambapo miundombinu yote ipo tayari kwa ajili ya kuanza.
0 Comments