




Na.Mwandishi Wetu
Maafisa Ushirika wametakiwa kusimamia matumizi ya Mfumo wa TEHAMA wa Usimamizi wa vyama vya Ushirika 'MUVU' kwa lengo la kuhakikisha mnyororo wa uzalishaji na ukusanyaji wa mazao unafanyika kwa usahihi na Mkulima anapata malipo sahihi na kwa wakati.
Ameyasema hayo Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika anayesimamia Masoko na Uwekezaji, Revocatus Nyagiro, wakati wa kikao cha mafunzo ya Usimamizi wa Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa Maafisa Ushirika na Watendaji wa Vyama yaliyoratibiwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa lengo la kukuza uelewa wa matumizi ya Mfumo huo kilichofanyika Bukoba Mkoani Kagera Juni 19, 2023.
Amefafanua kuwa ni wajibu wa Maafisa Ushirika kuhakikisha kuwa wanawapa watendaji wa Vyama vya Ushirika ushirikiano wa kutosha wa kutumia na kuelewa Mfumo huo wa Usimamizi katika hatua za ukusanyaji wa mazao kutoka kwa wakulima, uandaaji wa taarifa sahihi za mazao kwenye ghala, uuzaji na mkulima kupata mrejesho katika kila hatua kwa njia ya ujumbe mfupi wa Simu.
0 Comments